METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 23, 2016

Naibu Meya wa Dar Kupatikana kabla ya Pasaka


Baada ya kumpata Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mchakato wa kumchagua naibu meya umeanza.

Juzi, Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), Isaya Mwita alichaguliwa kuwa umeya akimshinda mpinzani wake Yusuph Yenga (CCM) kwa kura 84 dhidi ya 67.

Akizungumza jana, Meya Mwita alisema tarehe rasmi ya uchaguzi wa kumpata naibu meya haijafahamika na kwamba leo atashauriana na uongozi wa jiji na kwamba mara tu baada ya Sikukuu ya Pasaka ataitisha kikao cha baraza.

Mchakato wa kumpata naibu meya ni tofauti kwani idadi ya wajumbe watakaopiga ni ndogo ikilinganishwa na ile ya juzi ambayo madiwani wote na wabunge wote wa Mkoa wa Dar es Salaam walipigakura.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe alisema jana kuwa wajumbe watakaomchagua naibu meya hawatazidi 25 kutokana na kanuni zilizopo .

Alisema naibu meya atapatikana katika kikao cha kwanza cha Baraza kitakachoongozwa na meya.

Alisema wajumbe watakaoshiriki kikao hicho ni wabunge wa majimbo, kila manispaa; Ilala, Temeke na Kinondoni itatoa wajumbe watatu watakaoteuliwa na mameya wao na Meya wa Jiji atateua watatu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com