Mwenyekiti
wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Kanga Meternity Trust (KMT) Dkt. Mohd
Hafidh akitoa maelezo ya taasisi hiyo inavyofanya kazi zake kuhakikisha
Mama wajawazito wanapata huduma bora wanapokwenda kujifungua hospitali
Kuu ya Mnazimmoja katika hafla ya kuwasilishwa Utafiti wa Mradi wa
PartoMa iliyofanyika Hoteli ya Tembo, Forodhani Mjini Zanzibar.
Madaktari
bingwa wa Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Naufal Kassim (kushoto), Dkt.
Zaki (kati) na Mwenyekiti wa KMT Dkt. Mohd Hafidh wakijadiliana jambo
wakati wa hafla ya kuwasilishwa utafiti uliofanywa na Dkt. Anna Maaloe
(hayupo pichani) kuhusu wadi za wazazi za Hospitali ya Mnazimmoja.
Mtafiti
kutoka Mradi wa PartoMa Dkt. Anna Maaloe akiwasilisha utafiti wake juu
ya huduma za wodi za wazazi za Hospitali kuu ya Mnazimmoja katika hafla
iliyofanyika Hoteli ya Tembo Forodhani Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Baraza la wauguzi na wakunga Dkt. Amina Abdulkadir akitoa mchango
wake wakati wa kuwasilishwa utafiti wa huduma za wodi za wazazi za
Hospitali kuu ya Mnazimmoja. Picha na Makam Mshenga-Maelezo Zanzibar.(P.T)
Dkt. Ali
Salum kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali kuu ya Mnazimmoja
akimkabidhi cheti na zawadi Metroni Mkuu wa Hospitali hiyo kwa
kushiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Mradi wa PartoMa
katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Tembo.
Wauguzi
wa wodi ya wazazi katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja wakimpa zawadi ya
mlango na kasha Dkt. Anna Maaloe kwa kazi nzuri aliyosimamia ya utafiti
wa wodi za wazazi katika Hospitali ya Mnazimmoja. Picha na Makam
Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
Mradi wa
PartoMa unaoshirikisha Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini Denmark na
Hospitali Kuu ya Mnazimmoja wenye lengo la kuongeza ufanisi na
kuwajengea uwezo wafanyakazi wa wodi za wazazi katika hospitali ya
Mnazimmoja umeanza kuleta mafanikio makubwa.
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na mradi wa PartoMa kwa kushirikiana na
Taasisi isiyo ya kiserikali Kanga Martenity Trust (KMT) iliyopo
Hospitali ya Mnazimmoja umeonyesha vifo vinavyotokana na uzazi na
vifo vya watoto wanaozaliwa vimepungua tokea kuanza kwa mradi huo mwaka
mmoja uliopita.
Akiwasilisha
utafiti uliofanywa na mradi wa PartoMa ambao uliwashirikisha
madaktari, wakunga na wasaidizi wakunga katika wodi za wazazi, Dkt. Anna
Maaloe amesema bado ni mapema kuthibitisha kuwa mafanikio hayo
yanatokana moja kwa moja na kuwepo mradi huo lakini ufanisi na utaalamu
wa wafanyakazi kwenye wodi za wazazi Hospitali ya Mnazimmoja
umeongezeka.
Amesema
Hospitali za rufaa, kama ya Mnazimmoja zinawajibu mkubwa wa kuwa na
mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi waliopo na wanaotegemewa siku
za mbele na kuweka miongozo bora ili kuokoa maisha ya mzazi na mtoto
pamoja na wagonjwa wa kawaida.
“Kwa
kuliona hilo mradi wa PartoMa umekuwa ukiandaa mafunzo ya kuwajengea
uwezo madaktari na watendaji wa wodi za wazazi Hospitali Mnazimmoja
siku moja kwa miezi mitatu baada ya saa za kazi na kuweka miongozo
ambapo wafanyakazi wengi wamekuwa wakishiriki,” aliongeza Dkt. Anna.
Katika
utafiti huo Dkt. Anna amesema imebainika kuwa wafanyakazi wengi wa
Hospitali ya Mnazimmoja wamehamasika kuongeza elimu na ufanisi na hiyo
inasaidia katika kuokoa maisha ya wananchi.
Hata
hivyo amesema bado kunachangamoto katika kutoa huduma bora zaidi katika
Hospitali ya Mnazimmoja ikiwemo uhaba wa wafanyakazi katika wodi za
wazazi ukilinganisha na ongezeko kubwa la wazazi wanaotumia Hospitali
hiyo.
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyofanyika Hoteli ya Tembo Forodhani, Mwenyekiti wa
KMT Dkt. Mohammed Hafidh amesema utafiti huo ambao ni wa kwanza
kufanywa na kuwashirikisha watafiti wa wazalendo Hospitali ya
Mnazimmoja utasaidia kuwa na taarifa sahihi na za uhakika kwa maendeleo
ya Hospitali hiyo.
Amesema
lengo la utafiti huo ni kuwasaidia mama wajawazito kujifungua salama na
kwa heshma na kuzuia vifo vya mama na mtoto ambavyo vinaweza kuzuilika.
Nae Dkt.
Naufal Kassim amekiri kuwepo mtafartoMa na ameshauri madaktari
kujipanga kufanya tafiti zaidi za afya na kuyatumia matokeo ya tafiti
zilizopo kwa ukamilifu.
Katika
hafla hiyo Dkt. Ali Salum kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja aliwakabidhi vyeti madaktari, wakunga na wasaidizi wakunga
walioshiriki mafunzo ya kuwajngea uwezo baada ya saa za kazi bila
malipo katika hospitali hiyo.
0 comments:
Post a Comment