Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekatisha ziara yake ya siku sita mkoani
Simiyu, baada ya kifo cha ghafla cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
(DED), Trasias Kagenzi kilichotokea juzi usiku.
Kaimu Katibu
Tawala, Donatus Weginah alithibitisha kutokea kifo cha mkurugenzi huyo
wakati Waziri Mkuu akiwa na ratiba ya kutembelea wilaya hiyo.
Weginah
alisema juzi asubuhi Kagenzi alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia akiwa
na mlinzi wake na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Rosemary Kirigini lakini
alianza kujisikia vibaya.
“Mkurugenzi alikuwa akifanya mazoezi
‘jogging’ na DC Rosemary Kirigini, lakini baadaye alimwambia Kirigini
najisikia pumzi zinabana, akamwambia aendelee… lakini mara mkuu wa
wilaya alimuona amejiinamia, aliporudi kumuuliza akamwambia naona nakosa
hewa, ndipo alipoamua kukimbia kuchukua gari kumpeleka
hospitalini,”alisema.
Weginah alisema mkurugenzi huyo alipelekwa
hospitali na majira ya saa tano asubuhi alionekana akiendelea vizuri,
hata hivyo baadaye hali ikabadilika mchana na waliamua kumpeleka katika
Hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi, lakini usiku wa saa saba
alifariki dunia.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Tawala huyo, alisema
mkurugenzi ana kama mwaka mmoja na nusu tangu alipohamia wilayani humo
na kwamba familia yake iko Arusha.
0 comments:
Post a Comment