Viongozi
wa Ufaransa Hollande, Ugiriki Alexis Tsipras na Ujerumani Angela Merkel
wamejaribu kuendeleza mkataba kwa kutafutia suluhu mgogoro wa wahamiaji
katika bara la Ulaya, pamoja na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa
Ulaya.
Na RFI
Alhamisi
hii, MAchi 17, nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya wamefanya mazungumzo
na Uturuki. Lengo ni kukamilisha maelezo ya mkataba unaotakiwa kuzuia
wimbi la wahamiaji wanaoingia Ulaya. Mkataba ambao maudhui yake
yalielezwa wiki mbili zilizopita.
Hakuna
jipya ambalo limetoka kwa sasakatika kikao hiki cha kwanza cha
mazungumzo, amearifu mwandishi wetu katika mji wa Brussels, Juliette
Gheerbrant. Hata hivyo, shughuli katika makundi madogo zimefanyika kabla
ya ufunguzi mkutano huo. Rais wa Ufaransa amekutana na Kansela wa
Ujerumani na Waziri Mkuu wa Ugiriki kwa muda wa saa moja Alhamisi
asubuhi. "Mjadala wenye lengo la kujenga," wasaidizi wa Rais François
Hollande wamebainisha.
Ni wazi
kwamba utaratibu wa kuwarejesha wakimbizi nchini Uturuki unapaswa
kutekelezwa, itabidi Ugiriki uwezo wa kutosha ili kutathmini ombi la
hifadhi la kila mhamiaji. Alexis Tsipras pia amekumbuka wakati
alipowawasili katika Baraza la Ulaya kuwa nchi yake inahitaji msaada.
Waziri Mkuu wa Ugiriki ameelezea hali inayojiri katika kambi ya
wakimbizi ya Idomeni, kwenye mpaka wa kaskazini mwa nchi hiyo, ambapo
maelfu ya wahamiaji wameshikiliwa katika hali mbaya kutokana na kufungwa
kwa mpaka wa Makedonia. kwa mujibu wa Alexis Tsipras, hali hii ni aibu
kwa utamaduni wa Ulaya na itakuwa kuchukua maamuzi kwa ajili ya
kutafutia ufumbuzi, kuwasaidi na kuwalindia usalama kwa wakimbizi,
lakini pia kuharakisha zoezi la kuwahamisha.
Itakumbuka kwamba, rasimu ya makubaliano na Uturuki inatoa mambo kadhaa:
► kuongeza mara dufu kiasi cha Dola bilioni 3 (ambazo tayari zimetengwa kwaz ajili ya wahamiaji nchini Uturuki)
► Kufuta, kuanzia majira haya, mahitaji ya visa ya muda mfupi kwa raia wa Uturuki wanaoelekea Ulaya
►
kubadilishana kati ya mhamiaji na mkimbizi, ikimaanisha mhamiaji
alieingia kinyume cha sheria nchini Ugiriki 9 kumrejesha Uturuki) dhidi
ya mkimbizi anaeishi nchini Uturuki( kwa kwenda Ulaya)
► kuongeza kasi ya mazungumzo kwa ajili ya kuingizwa kikamilifu kwa Uturuki katika Umoja wa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment