SERIKALI imesema itatoa bei elekezi
katika sekta ya afya hivi karibuni baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kubariki bei hizo kuanza kutumika kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wa gharama
wananchi.
Bei elekezi kwa vituo vya afya
zimeshasainiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
na baadhi ya vituo vya afya vimeshaanza kutumia bei hiyo.
Aidha, serikali imepanga kuweka
utaratibu wa wagonjwa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa
ni hatua ya kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangalla wakati
akizungumza na waaandishi wa habari baada ya kuzindua Matokeo ya Utafiti wa
Kutathimini utoaji wa huduma za afya nchini kwa mwaka 2014/2015.
“Bei elekezi ziko mbioni kutoka na
baadhi ya vituo wameshaanza kuzitumia kwa sababu zimeshasainiwa na Waziri, sasa
hivi tunasubiri Baraka za Waziri Mkuu akiziridhia tutazitangaza rasmi,” alisema Dk Kigwangalla.
0 comments:
Post a Comment