Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) akipata taarifa ya utendaji wa
Shirika la Posta Tanzania (TPC) kutoka kwa Meneja Mkoa wa Mwanza Bw.
Julius Chifungo (katikati) wakati alipotembelea ofisi za Shirika hilo
jijini Mwanza. Kulia ni Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza, Johnbosco
Kalista.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia)
akipata maelezo ya namna mitambo ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
inavyofanya kazi kutoka kwa Mtaalamu wa Mitambo (Technician) Edward
Lukungu (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya kutembelea Shirika hilo
jijini Mwanza.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka
watendaji wa Shirika la Posta Tanzania na Kampuni ya simu ya (TTCL)
kufanya kazi kwa weledi na mtazamo wa kibiashara ili kuyaongezea
mapato mashirika hayo na hivyo kuendana na mabadiliko ya sayansi na
teknolojia yanaoyotokea nchini.
Akizungumza
na wafanyakazi wa TTCL na POSTA mkoani Mwanza Prof. Mbarawa amesema
kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano duniani biashara simu na
posta hivi sasa ina ushindani mkubwa unaohitaji mtazamo mpana wa
kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko.
“Serikali
inajitahidi kuisaidia TTCL na POSTA hivyo wekezeni vizuri kwenye data
na uharaka wa utoaji huduma ili muweze kushindana kwenye soko na kukuza
uchumi wa taasisi hizi muhimu kwa usitawi wa nchi”, amesema Prof
Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amezitaka menejimenti za POSTA na TTCL kufanya kazi kwa uwazi na
uadilifu ili malengo na mikakati ya taasisi hizo yafahamike kwa
wafanyakazi wote na kuwezesha kujipima kama wanafikia malengo
yaliyokusudiwa.
“Hakikisheni
wafanyakazi wote wanaelewa malengo na mikakati ya tasisi zenu ili kazi
ya kuyatekeleza ifanywe kwa umoja na ushirikiano”, amesisitiza Waziri
Prof. Mbarawa.
Aidha,
Waziri Prof. Mbarawa amesisitiza umuhimu wa wafanyakazi kuwa wadilifu na
kuepuka kuwa mawakala wa mashirika mengine na hivyo kuihujumu Serikali.
“kuna
watu ndani ya TTCL na POSTA ambao ni wazembe, wavivu na wanao hujumu
Serikali tutawaondoa mara moja, Ni vema kubaki na wafanyakazi wachache
waadilifu kuliko wengi wasiotimiza maelngo yaliyokusudiwa”, amefafanua
Waziri Prof. Mbarawa
Naye
Meneja wa TTCL mkoa wa Mwanza Bw. Johnbosco Kalista amemweleza Waziri
Mbarawa kuwa wigo wa mtandao kutofikia walaji wengi, wateja kutolipa
madeni kwa wakati na ulinzi na usalama wa miundombinu ya mawasiliano ni
miongoni mwa changamoto zinazoikabili shirika hilo mkoani Mwanza.
Kwa
upande wake Meneja wa POSTA mkoa wa Mwanza, Bw. Julius Chifungo
amebainisha kuwa uchakavu wa barabara, maslahi yasiyokidhi ya
wafanyakazi na uchakavu wa majengo ni miongoni mwa vikwazo vinavyoathiri
utendaji kazi wa shirika hilo mkoani Mwanza.
Takribani
masanduku elfu tisa yanasimamiwa na Shirika la Posta mkoani Mwanza
katika ofisi zake kumi na moja na asilimia 96.8 hukodishwa na kuingizia
shirika hilo faida, Wakati takriban wateja 45,041 wanahudumiwa na TTCL
katika Mkoa wa Mwanza.
0 comments:
Post a Comment