METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, December 30, 2015

MIMBA ZA UTOTONI ZA MKERA DC MAKONDA ACHACHAMAA…!!!

 
 
DAR ES SALAAM

MKUU wa wilaya ya Kinondoni,Mhe Paul Makonda amewataka wakazi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 5/1 mwakani kwa ajili ya kushirikiana kwa pamoja katika ujenzi wa shule 6 za Sekondari wilayani humo ili kupunguza wimbi la vijana wanaokaa bure bila kwenda shule kwa kisingizio cha shule kuwa mbali.
DC Makonda amesema kuwa suala hilo pia litasaidia katika kupunguza mimba za utotoni na maambukizi ya virusi vya ukimwI.
 
 

Njia bora ya kumsaidia maskini ni kumsomesha mtoto wake. Nawaomba watu wote wenye mapenzi mema tuungane kujenga Secondary 6 ktk Wilaya yetu ya Kinondoni ili kuwezesha vijana zaidi ya 3183 kuendelea na masomo yao. Kazi ya ujenzi inaanza tareh 5/1/2016. Kwa kufanya hivi tutawaokoa vijana hawa na Mimba za utotoni, Magonjwa, matumizi ya madawa la kulevya na hata ukabaji. Nawaomba tena tuunganishe nguvu zetu. 
 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com