Bendera ya Palestina ikipandishwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 30, 2015
Jumatano
hii, Septemba 30, bendera ya Palestina imepandishwa kawa mara ya kwanza
mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Palestina
iliteuliwa mwaka 2012 kuwa mwangalizi katika Umoja wa Mataifa, lakini
ilichukua hadi katikati mwa mwezi Septemba ili kuruhusu bendera yake
kuelea mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Bendera
hii ya Palesyina yenye rangi nyekundu, nyeusi, nyeupe na kijani
imepandishwa saa 7:15 (sawana saa 11:15 jioni saa za kimataifa) katika
bustani ya taasisi ya kimataifa, na toka leo Jumatano itakua sambamba na
bendera193 za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Vatican,
ambayo, kama Palestina, inatambuliwa kama taifa lisilokuwa mwanachama.
" Katika
wakati huu wa kihistoria, ninawaambia watu wangu kila mahali pandisha
juu kabisa bendera ya Palestina, kwa sababu ni ishara ya utambulisho
wetu. Hii ni siku ya kujisifu ", amesema Rais wa Palestina Mahmoud
Abbas, mapema katika sherehe iliyohudhuriwa na mamia ya watu, ikiwa ni
pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Abbas,
muda mfupi kabla alitangaza katika jukwaa la Mkutano Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, kwamba Palestina inatakiwa kutambuliwa kama taifa huru
linalojitegemea.
Huu ni
ushindi wa kidiplomasia kwa mamlaka ya Palestina, lakini jambo hili
linashutumiwa na wawakilishi wa Israel katika Umoja wa Mataifa. Katika
Majimbo Yanayokaliwa, wakati baadhi ya wanakaribisha hatua hii mpya
kuelekea kutambuliwa kimataifa kwa taifa la Palestina, watu wengi
wanajua kwambahali hii haitoleta mabadiliko katika maisha yao ya kila
siku.
Vita
nchini Syria, harakati za makundi ya kigaidi au mgogoro wa wahamiaji
vinawatia wasiwasi viongozi na marais wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa
Umoja wa Mataifa mjini New York, sawa na hali inayoendelea katika
majimbo ya Gaza na Cisjordania, amearifu mwandishi wetu nchini Marekani,
Anne Corpet, ambaye amekumbusha kwamba sababu ya Palestina, kuwepo
katika mkutano huo, kumepelekea iwekwe katika agenda ya Mkutano Mkuu wa
Umoja wa Mataifa wa Mwaka huu.
Kwa
karibu miaka 70, suala la Palestina lilipelekea kuchukuliwa maazimio
mengi katika Umoja wa Mataifa, ambapo ilipewa kipaumbele katika mijadala
mbalimbali. Baadhi ya maazimio hayo licha ya kuwa ni machache
yalitekelezwa, na miradi mingi ilijikuta ikikabiliwa na upinzani mkubwa
wa kura ya turufu ya Marekani. Katika hotuba inayosubiriwa sana kwenye
jukwa la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jumatano wiki hii, Rais wa
Mamlaka ya Palestina atachukua nafasi hiyo kwa kuiomba jumuiya ya
kimataifa kuchangia juu ya hatma ya watu wake.
0 comments:
Post a Comment