Jimbo la Iringa
Mjini
MKUU
wa wilaya ya Wanging’ombe, Frederick Mwakalebela ameibuka kidedea katika kura
za maoni za kutafuta kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Iringa Mjini kwa
kuwabwaga vibaya washindani wenzake 12.
Mmoja
wa wagombea aliyebwaga katika kura hizo ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa,
Jesca Msambatavangu aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa mshindi kwa
kuzingatia nafasi aliyonayo ndani ya chama na nguvu yake kisiasa mjini Iringa.
Katika
kura hizo, Mwakalebela alipata kura 4,388 huku Msambatavangu akijinyakulia kura
2,077 zilizompa ushindi wa pili, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Dk Yahaya Msigwa
aliyepata kura 1,097.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo, Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Elisha Mwampashi
aliwataja wengine na kura zao kwenye mabano kuwa ni Dk Augustino Maiga (745),
Mahamudu Madenge (423), Addo Mwasongwe (259), Nuru Hepautwa (191), Frank Kibiki
(183), Michael Mlowe (183), Fales Kibasa (171), Aidan Kiponda (135), Peter Mwanilwa
(79) na Agustino Mwilonge (66).
Jimbo la Isimani
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametetea nafasi yake
baada ya kuzoa kura 10,799 kati ya kura 12,560 zilizopigwa.
Lukuvi
alifuatiwa kwa mbali na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Festo Kiswaga aliyejipatia
kura 1,237.
Katibu
wa CCM Iringa Vijijini, Dodo Sambu aliwataja wengine na kura zao kwenye mabano
kuwa ni Hamis Malinga (323), Sebastian Kiyoyo (155), , Elias Luputiko (62).
Jimbo la Kalenga
Matumaini
ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kuwatumikia wananchi wa jimbo la
Kalenga kwa kupitia nafasi ya ubunge huenda yakawa yamepotea kabisa baada ya
kuambulia kura 674 kati ya kura 22,253 zilizopigwa.
Hii
ni mara ya pili kwa Kandoro kuonesha nia ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo bila
mafanikio, mara ya kwanza ikiwa ni katika kura za maoni za 2010 alipoambulia kura 2,353 dhidi ya kura 2,819
alizopata aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk William Mgimwa.
Katibu
wa CCM Iringa Vijijini Dodo Sambu alimtaja mshindi wa kura hizo za maoni kuwa
ni mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake, Godfrey Mgimwa aliyezoa kura
15,550.
Wengine
na kura zao kwenye mabano ni Jackson Kiswaga (3,439), George Mlawa (301) na
Kibasa Kibasa (289).
Jimbo la Mafinga
Mjini
Afisa
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Cosato Chumi ameibuka
mshindi kwa kuzoa kura 3,683.
Chumi
amaye ushindi wake ulidhihiri kujionesha mara tu baada ya kutangaza nia ya
kuwani ubunge katika jimbo hilo hivikaribuni, alifuatiwa kwa mbali na Zuberi
Ngullo aliyepata kura 700 huku James Mgimwa akipata kura 378, Benjamin Balali
kura 302 na Paulo Muyinga akiambulia kura 19.
Jimbo la Mufindi
Kaskazini na Mufindi Kusini
Hadi
tunakwenda mitambo zoezi la kuhesabu kura lilikuwa likiendelea huku taarifa za
awali zikionesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamudu Mgimwa kuibuka
mshindi katika jimbo lake la Mufindi Kaskazini.
Huko
Mufindi Kusini, taarifa za awali zinaonesha kumpa ushindi mbunge anayemaliza
muda wake, Mendrad Kigola.
Jimbo la Kilolo
Hadi
tunakwenda mitambani hakukuwepo na taarifa rasmi za matokeo ya jimbo hilo
japokuwa wapambe wa wagombea wawili kati ya 15 waliojitokeza kuwania jimbo hilo,
wamejitapa kushinda kura hizo za maoni.
Wakati
wapambe wa mbunge anayemaliza muda wake, Profesa Peter Msolla wakidai kupata
ushindi wa kishindo wa kura zaidi ya 13,000 nao wapambe wa Mkuu wa Wilaya ya
Kaliua Tabora, Venance Mwamoto wanadai mgombea wao ameshinda japokuwa
hawakutaja idadi ya kura walizopata.
0 comments:
Post a Comment