MABINGWA
wa zamani wa Afrika, TP Mazembe, wanatarajiwa kutua nchini kesho ambapo
pamoja na mambo mengine, watawachunguza kwa karibu zaidi nyota kadhaa
waliotamba kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika wiki
iliyopita jijini Dar es Salaam, wakiwamo Geoffrey Mwashiuya na Malimi
Busungu wa Yanga.
Miamba
hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imeonekana kuvutiwa na
wachezajihao kutokana na viwango vyao, wakiwamo Pascal Wawa, Mussa Farid
na wengineo wa Azam.
Mtu wa
karibu na timu hiyo wanayochezea Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu, alisema kuwa mabosi wa TP Mazembe wamevutiwa na baadhi ya
wachezaji wa Yanga na Azam waliocheza Kagame wakipata picha kuwa
Tanzania imesheheni vipaji vya soka hivyo ni vema wakaelekeza nguvu zao
ili kuviendeleza.
“Kombe la
Kagame ni neema kwa wachezaji wa Tanzania, (mabosi wa TP Mazembe)
walikuwa wakifuatilia sana mashindano hayo na kugundua vipaji vingi tu,
wakiwamo Busungu, Geoffrey, Deus Kaseke pamoja na wengine kutoka Azam,
wakimtaja pia Wawa raia wa Ivory Coast,” alisema mtoa habari wetu huyo
ambaye hakutaka jina lake kuwekwa hadharani.
0 comments:
Post a Comment