TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ofisi ya
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasikitika kuwepo
kwa taarifa za uzushi ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii
zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu
msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Habari
hizi si za kweli na tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa
Makamu wa Rais, hausiki na taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya
Kijamii na wala hajapanga tukio lolote la kukutana na waandishi wa
habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali
na Chama Cha Mapinduzi.
Aidha
tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa
zisizo sahihi kwa maslahi yao waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa
kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na
kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyohusika na kutambulika.
Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
10/8/2015
0 comments:
Post a Comment