WILAYA
ya Mufindi ni moja kati ya wilaya saba nchini zitakazoanza kuzalisha viazi
lishe vyenye asilimia kubwa ya vitamin A ikilinganishwa na aina nyingine ya
vyakula vya mbogamboga, matunda na mizizi.
Mbali
na Mufindi, wilaya zingine zilizoingizwa katika mpango huo na shirika la kimataifa
linaloshughulikia mazao ya viazi (CIP) ni pamoja na Iringa, Ulanga, Mbozi,
Chunya, Gairo na Wanging’ombe.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi, Ndimmyake Mwakapiso alisema viazi hivyo ni aina ya viazi vitamu vyenye
rangi ya chungwa.
Alisema
viazi hivyo vina asilimia 90 ya vitamini “A” inavyohitajika katika mwili wa
binadamu ili kumuwezesha kuwa na uwezo mzuri wa kuona, kujenga ubongo wa watoto
chini ya miaka mitano na kuimarisha afya ya wajawazito.
Alisema,
mradi huo umeanza kutekelezwa kupitia vikundi vya wakulima vinavyootoesha mbegu
kwenye maeneo yenye miundombinu ya umwagiliaji.
Maeneo
hayo yapo katika viijiji vya Igomaaa na Lugolofu pamoja bustani ambazo
hutambulika kwa jina la vinyungu zilizopo kwenye vijiji vya Lugema, Mabaoni na
Makungu.
Mwakapiso
alisema mbegu zitakazozalishwa zitagawiwa kwenye vijiji 18 ambayo vimechaguliwa
kuanza kutekeleza mradi huo baada ya msimu wa mvua kuanza.
“Vijiji vitakavyo pata mbegu hizo ni Makungu,
Mabaoni, Lugema, lugolofu, Iramba,
Ikimilinzowo, Nyigo, Nyanyembe, Maguvani, Idetero, Mkangwe, Ikangawani na
Idumulavani, Igomaa, Utosi, Kibada,
Ugenza na Ikweha”, alisema.
Alisema
viazi vikizalishwa kwa wingi na kuongezwa thamani ya zao hilo vitamwongezea mkulima
kipato kwani soko lake linapatikana kwa urahisi huku vikiwa na uwezo wa
kuzindikwa kwa kutengeneza Kripsi, Mikate, Chapati, Biskuti, juisi na Unga wa
lishe.
Aliwataka
wakulima watakaopata mbegu hizo wazitumie vizuri ili uzalishaji wa zao hilo ulete
matokeo yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na hatimaye kuwaondoa katika
umasikini.
0 comments:
Post a Comment