METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, August 3, 2015

KURA YA MAONI KUAHIRISHWA KILOLO.....


PRO. Msola akivalishwa kofia

Chama Cha mapinduzi ( CCM) Wilaya ya kilolo mkoani Iringa kimefuta
matokeo ya kata tatu ambayo ni feki yaliyokuwa yakimpa ushindi mkubwa
mbunge anaemaliza muda wake Prof Peter Msola

Matokeo hayo ambayo yamekataliwa na wagombea wote yanadaiwa kupachikwa
ktk vituo vya kata hizo tatu japo hata hivyo hayana uhalisia
ukilinganisha na idadi ya wanachama wa maeneo husika

Chanzo cha ndani na baadhi ya wagombea walioshindwa wameueleza mtandao
huu wa www.matukiodaima.co.tz kuwa walishangazwa kuona ghafla mbunge
Prof Msola akiongoza katika vituo vya kata hizo ambazo hata matokeo Yake
hayakusainiwa na mawakala wa wagombea wengine na ndizo kata ambazo
matokeo Yake yalikuwa na utata

Kwani walisema kimsingi matokeo halali ya kata zaidi ya 5 Mwamoto ndie
alikuwa akiongoza kwa kura nyingi zaidi kuliko za mgombea mwingine
yeyote huku mbunge anaemaliza muda wake akimfukuza kwa mbali sana

Bila kutaja matokeo hayo kwa kuwa si wasimamizi wakuu wa uchaguzi huo
walisema walitegemea matokeo ya jumla Mshindi kuwa Mwamoto ila ilitaka
kuwa tofauti kwa ambae hakuongoza ktk vituo kutaka kuongoza kwa matokeo
ya jumla hivyo kulazimika kuchunguza matokeo hayo na kubaini Wizi huo .

Kwani ktk vituo idadi ya kura ni nyingi kuliko ile ya wanachama na
wakazi wa eneo husika hata kama wana kijiji wote hadi watoto wa mwaka
mmoja wangepiga kura bado kura zilikuwa nyingi  kuliko wakazi wa eneo
husika

Alisema kosa walilolifanya ni kuongeza idadi ya kura za mbunge Prof
Msola bila kufuta idadi ya kura za Mwamoto ama idadi ya wapiga kura ya
jumla

Hivyo ukitazama idadi halisi ya wapiga kura ,kura zilizopigwa na kura
zilizoharibika bado ni vitu viwili tofauti na kufananisha Wizi huo ni
sawa na Wizi bila mahesabu.

Pia ktk hali ya kushangaza ni kuona matokeo halisi ya uchaguzi huo
yakiyangazwa katika mitandao ya kijamii kuwa Prof Msola amepata kura
13,000 huku Mwamoto akipata kura 8000
Wakati bado hata kura kuhesabiwa.

Taarifa ya chama Wilaya iliyotolewa kwa vyombo vya habari imepinga
vikali matokeo hayo kuwa ni feki.

"Hayo matokeo ni ya kwake wala si yajimbo la kilolo halafu anaepaswa
kutoa matoke ni katibu wa chama na si vinginevyo siyo mwandishi wa
habari wa Mgombea na endapo mtu anaweza kutoa makeo au kwa idhini ya
ofisi wilaya naanisha katibu wa ccm wilaya huu. Ukweli ni kwamba matokeo
ya jimbo la kilolo hayajatangazwa sababu, uchaguzi utarudiwa katika kata
tatu kunadosari zimejitokeza. Hiyo taarifa rasimi toka jimbo la kilolo
na wilaya ya kilolo CCM Oyeeeeeeeee" ni taarifa iliyotolewa na CCM
Wilaya ya Kilolo

Hadi sasa uchaguzi katika kata hizo tatu ni siku ya Jumanne ndipo
matokeo halisi yatatangazwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com