HALMASHAURI
Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa imefanya uteuzi wa wagombea
udiwani katika kata za majimbo yote huku ikithibitisha kumkata Mwenyekiti wa
CCM wilaya ya Mufindi, Yohanes Kaguo.
Kaguo
aliyekuwa diwani wa Kata ya Makungu wilayani Mufindi katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita amekatwa baada ya kushindwa kura za maoni za kata hiyo.
Katika
kura hizo za maoni, Kaguo anayeelekea kupotoza ushawishi ndani ya chama hicho
alipata kura 351 dhidi ya kura 465 alizopata Kizito Kambo.
“Kwa
matokeo hayo halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Iringa inampendekeza Kizito Kambo
kuwa mgombea udiwani katika kata hiyo,” alisema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Iringa, Jesca Msambatavangu huku wajumbe wengine wakiafiki uteuzi huo.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi anayemaliza muda wake, Peter
Tweve alinusurika kukatwa katika kikao hicho kichofanye uteuzi wa wagombea wa
kata 37 za wilaya ya Mufindi baada ya mmoja wa wajumbe kuingiza hoja
inayomuhusisha na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.
Mmoja
wa wajumbe wa kikao hicho (hakutaja jina) alisema Tweve aliyeshinda kwa mara
nyingine tena kura za maoni za kata yake ya Kiyowela anatuhumiwa kwa matumizi
mabaya ya fedha za halmashauri hiyo.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa alimuokoa diwani huyo akisema; “hatuwezi kumuhukumu mtu kwa tuhuma,
tumesikia tuhuma hizo na kama bado zipo atawajibika kwa nafasi yake, hatuwezi
kufanyia kazi tuhuma mpaka mtu ahukumiwe.”
Katika
jimbo la Iringa Mjini wagombea wa kata 18 waliteuliwa akiwemo Farida Mpogole wa
kata ya Mtwivila ambaye viongozi wa CCM Iringa Mjini walimrushia tuhuma
zinazomuhusisha kuwa na mahusiano ya jirani na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini
anayemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa.
Mwingine
aliyepitishwa Iringa Mjini ni Benjamini Chatanda wa kata ya Igumbilo
anayehusishwa na tuhuma za udanganyifu na matumizi ya fedha wakati wa kura hizo
za maoni.
Pamoja
na kuteua wagombea udiwani wa wilaya ya Mufindi na Iringa Mjini, kikao hicho
pia kiliteua wagombea wa kata 28 wa Iringa Vijijini na 24 wa wilaya ya Kilolo.
Baaada
ya hitimisho la uteuzi huo, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa alisema; “tuna kazi
kubwa mbele yetu, ule wimbo wetu wa wataisoma namba ili uwe kweli ni lazima
tujipange, vinginevyo tunaweza kuwa sisi CCM wa kusoma namba za watu, turudi
tukajipange.”
Alisema
ni jukumu la viongozi kuhakikisha wanarekebisha hali ya hewa kwa kusaidia
kuvunja makundi, kama yapo, ili katika mchakato wa uchaguzi huo waende pamoja.
0 comments:
Post a Comment