METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 16, 2015

Mwandishi wa Habari Achukua fomu ya Ubunge kupitia ccm Iringa

Frenk Kibiki akisain kitabu cha wageni baada ya kuwasili  kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la iringa mjini hapa akiwa katika ofisi za ccm Iringa mjini



 Kibiki akisain kitabu hicho


Mgombea ubunge akifafanua mambo na adhima yake kwa waandishi wa habari na wananchi waliomsindikiza kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la iringa mjini hapa akiwa katika ofisi za ccm Iringa mjini



Mgombea ubunge akifafanua mambo na adhima yake kwa waandishi wa habari na wananchi waliomsindikiza kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la iringa mjini hapa akiwa katika ofisi za ccm Iringa mjini.(picha Na Mkakala Denis)

Mwandishi huyo ambaye ameanza kwakueleza ukweli wa maisha ya wakazi wa iringa ikiwa nayeye ameyaishi kwa muda sasa amesemakuwa kutokana na ugumu wa maisha ya wananchi wa mkoa huu umetokana na wananchi kutoeleza na kutopata kiongozi wa kuweza kumueleza Iringa ipi mwananchi huyo angehitaji kuishi kwa sasa na baada ya miaka kadhaa ijayo.
Vilevile kibiki amejinasibu kwakusema kwakuwa jamii inahitaji kiongozi inapswa kutumia uelewa zaidi ili kumtambua kiongozi anayefaa nasio kufuata watu wanasema nini na kufuata kipato cha mtu ikiwa wao bado wanaishi katika mazingira magumu hivyo inahitajika kumpata kiongozi anayetoka na maisha kama anayoishi mwanairinga wa sasa.
Hata hivyo Kibiki ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huu kutumia muda wao katika kusikiliza siasa zisizo za chuki ili kutambua nikiongozi yupi mwenye malengo na jimbo lao ikiwa mpaka kufikia hii leo wanachama zaidi ya 3 wameshachukua fomu za kugommbea nafasi hiyo huku wengine wakionyesha uwezo wa fedha na mali ikiwa wananchi wenyewe hawana mali hizo hivyo wananpaswa kutizama ni yupi anafaa ikiwa wengine wanahitaji madalaka ili kufurahisha nafsi na si kutatua matatizo ya jamii.
"mimi ni masikini mwenzenu kama ambavyo wengine wanavyoniita hivyo nahitaji kupeleka matatizo ya masikini wenzangu bunge ili kupigania na kuwa katika hali moja ya walionacho na wasionacho na kuondoa utofauti huo pia kuwatetea machinga na akina mamantilie na ambao hukimbizwa na migambo wa mji kila kukicha.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com