FRANK LEONARD (MMILIKI WA BLOG HII) AKIPOKEA TUZO YAKE TOKA KWA WAZIRI WA MALIASILIA NA UTALII LAZARO NYALANDU BAADA YA KUWA MSHINDI WA KWANZA WA UANDISHI BORA WA HABARI ZA UTALII WA NDANI KATIKA HAFLA ILIYOFANYIKA JANA JIJINI MWANZA. LEONARD AMBAYE NI MSHINDI KWA UPANDE WA MAGAZETI NCHINI AMEPATA CHETI, NGAO, SH MILIONI 2 NA ATAKWENDA SAFARI YA MAFUNZO KATIKA NCHI ZA SADC.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu aki mkabidhi tuzo maalum ya
heshima Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerari Sarakikya akiwa na mkewe kwa
kupanda mlima Kilimanjaro mara 38, Jenerari Sarakikya pia amepewa Kadi
maalum ya kuingia mbuga zozote za TANAPA Bure yeye pamoja na familia
yake lakini ambapo katika hatua nyingine atalipiwa gharama zote za
kushiriki mkutano wa masuala ya utalii kuhusu milima mirefu zaidi
duniani yeye pamoja na mke wake huko nchini Marekani, Katika mkutano
huo Jenerari Sarakikya anatarajiwa kutoa mada kuhusu mlima Kilimanjaro.
Jenerari
Mrisho Sarakikya amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla ya utoaji wa tuzo
za TANAPA za waandishi wa habari za utalii iliyofanyika kwenye hoteli
ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo ambapo waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali wamepewa tuzo hizo.
Katika
picha kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi
za mbuga za Taifa TANAPA.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANZA)
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akipiga picha ya pmaoja na washindi.
0 comments:
Post a Comment