METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 2, 2015

MSHINDI WA KWANZA WA UANDISHI BORA WA HABARI ZA UTALII WA NDANI


????????????????????????????????????
FRANK LEONARD (MMILIKI WA BLOG HII) AKIPOKEA TUZO YAKE TOKA KWA WAZIRI WA MALIASILIA NA UTALII LAZARO NYALANDU BAADA YA KUWA MSHINDI WA KWANZA WA UANDISHI BORA WA HABARI ZA UTALII WA NDANI KATIKA HAFLA ILIYOFANYIKA JANA JIJINI MWANZA. LEONARD AMBAYE NI MSHINDI KWA UPANDE WA MAGAZETI NCHINI AMEPATA CHETI, NGAO, SH MILIONI 2 NA ATAKWENDA SAFARI YA MAFUNZO KATIKA NCHI ZA SADC.

 ????????????????????????????????????

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu aki mkabidhi tuzo maalum ya heshima Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerari Sarakikya akiwa na mkewe kwa kupanda mlima Kilimanjaro mara 38, Jenerari Sarakikya pia  amepewa Kadi maalum ya kuingia mbuga zozote za TANAPA Bure yeye pamoja na familia yake lakini ambapo katika hatua nyingine  atalipiwa gharama zote za kushiriki mkutano wa masuala ya utalii kuhusu milima mirefu zaidi duniani  yeye pamoja na mke wake huko nchini Marekani, Katika mkutano huo Jenerari Sarakikya anatarajiwa kutoa  mada kuhusu mlima Kilimanjaro.
Jenerari Mrisho Sarakikya  amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari za utalii iliyofanyika kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo  ambapo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali  wamepewa tuzo hizo.
Katika picha kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANZA)
????????????????????????????????????
 
 
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akipiga picha ya pmaoja na washindi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com