BALOZI
Mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk Agustine Maiga ameingia katika kinyang’anyiro
cha kutafuta ridhaa ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili agombee
ubunge katika jimbo la Iringa Mjini.
Kabla
ya kuingia katika kinyang’anyiro hicho, Dk Maiga alikuwa mmoja kati ya wana CCM
38 waliokuwa wakitafuta ridhaa ya chama hicho ili awanie urais; mchakato huo ulihitimishwa
kwa kumchagua Dk John Pombe Magufuli kupeperusha bendera ya chama hicho.
Dk
Magufuli, Dk Maiga na Jaji Augustino Ramadhani ni baadhi ya wana CCM waliotajwa
mara baada ya sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika mwaka huu mjini
Songea, kwamba uadilifu walionao unawabeba kurithi nafasi hiyo kutoka kwa Rais
Jakaya Kikwete.
Mbali
na Dk Maiga, wana CCM wengine 12 wametajwa na Katibu wa CCM wa wilaya ya Iringa
Elisha Mwampashi kuchukua fomu za kuwania kugombea nafasi hiyo.
Wana
CCM hao ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu, Mkuu
wa Wilaya ya Wanging’ombe Frederick Mwakalebala na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
CCM Taifa Mahamudu Madenge.
Katika
orodha hiyo yupo pia Dk Yahaya Msigwa, Nuru Hepautwa, Addo Mwasongwe, Adestino Mwilinge, Frank Kibiki, Aidani Kiponda,
Peter Mwanilwa, Fales Kibasa na Michael Mlowe.
Akizungumza
na wanahabari mara baada ya kurejesha fomu zake, Dk Maiga alisema; “mimi
nimerudi hapa nchini kuja kulitumikia Taifa langu katika ngazi yoyote ile ya
uongozi.”
Alisema
baada ya kufikiri na kupata ushauri kutoka katika makundi mbalimbali ya jamii,
ameamua kuingia katika mchakato huo akiwa na dhamira ile ile iliyomsukuma
kugombea urais ili ashirikiane na wana Iringa kuleta maendeleo.
Alisema
endapo atachaguliwa vipaumbele vyake vitakuwa ni kuzingatia mambo yanayojikita
katika biashara, uwekezaji, ujasiriamali, ajira kwa vijana, ustawi wa jamii
pamoja na kuboresha yale ambayo yamefanyika.
Alisema
mji wa Iringa una nafasi ya pekee katika uwekezaji kwani ni kiungo cha barabara
kuu zinazounganisha baadhi ya barabara kuu nchini na zile zinazokwenda nchi za
nje.
Kwa
kufungua barabara hizo alisema, Iringa itakuwa kiungo cha kuendeleza utalii
kusini mwa Tanzania ili ufikie kiwango cha ukanda wa kaskazini.
“Kama
miji yoyote inavyopanuka kwa haraka, Iringa itapanuka kwa haraka na moja kati
ya vipaumbele vyake itakuwa ni kujenga makazi ya kisasa,” alisema.
Dk Maiga alisema kuingia katika kinyang’anyiro
hicho, kwake yeye hiyo ni fursa ya pekee kwa kuzingatia kwamba jimbo la Iringa
Mjini limekuwa katika mikono ya upinzani kwa miaka mitano sasa.
Alisema
kwa kupitia jitihada mpya za kurudisha jimbo hilo mikononi mwa CCM, chama hicho
kina haja ya kuingiza mawazo mapya, uongozi mpya na kutathimini nini
kilichotokea ili yaliyotokea yasitokee tena.
Alisema katika siasa umoja ni ushidi na akaonya siasa isitumike kwa uhasama na rushwa ikataliwe kwani inadharirisha utu.
Alisema heshima CCM na wafuasi wa kutosha watarudi endapo makundi yaliyojengeka huko nyuma na kugawa chama yatamalizwa.
0 comments:
Post a Comment