Azam FC
jana wameweza kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya KCCA ya Uganda
kwenye mchezo wa kundi B michuano ya Kagame inayoendelea kutimua vumbi
jijini Dar es Salaam mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jioni ya
jana.
John
Bocco ‘Adebayor’ aliifungia Azam goli pekee lililoipa timu yake ushindi
mwanzoni wa kipindi cha kwanza. Baada ya ‘Wanalambalamba’ kupata goli
hilo walitawala kipindi hicho wakicheza soka la pasi nyingi fupifupi na
mara chache walipiga mipira mirefu.
Kipindi
cha kwanza kilimalizika Azam wakiwa mbele kwa goli 1-0 dhidi ya KCCA ya
Uganda ambayo ilitafuta kwa udi na uvumba goli la kusawazisha lakini
ukuta uliokuwa ukiongozwa na Pascal Wawa akisaidiana na Said Morad
pamoja na Agrey Morris ulikuwa haupitiki kirahisi.(P.T)
Kipindi
chapili hakikuwa kikali kama kipindi cha kwanza kwasababu timu zote
zilitengeneza mashambulizi machache, Azam wakilinda zaidi goli lao na
kutengeneza mashambulizi machache ya kuvizia.
Azam
walifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Kipre Tchetche, Jean Mugiraneza
pamoja na Mudathir Yahya lakini kuingia kwao hakukubadili matokeo kwani
hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika, Azam wakafanikiwa kuungana na
KMKM ya Tanzania visiwani kuibuka na ushindi baada ya wawakilishi
wengine wa Tanzania (Yanga) kupoteza mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Gor
Mahia ya Kenya.
0 comments:
Post a Comment