Sporting
Lisbon imemsajili kinda huyu anayejulikana kwa jina la Martunis ambaye
alinusurika kufa katika mafuriko ya Tsunami takribani miaka 11
iliyopita.
Sporting
Lisbon imemsajili mhanga aliyenusurika katika janga la mafuriko ya
Tsunami, Martunis kwenye akademi yao, ikiwa imepita miaka 11 tangu janga
hilo kutokea huku likisababisha vifo vya mama yake na kaka zake wawili.
Ikumbukwe tu Martunis aliweza kuishi ndani ya dimbwi la maji kwa
takribani siku 21.
Martunis,
ambaye kwa sasa ana miaka 11, ametambulishwa huko jijini Lisbon akiwa
tayari kabisa kutimiza ndoto zake licha ya kupitia misukosuko katika
jango hilo mwaka 2004.
Mawimbi
hayo makali, yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi katika bahari ya
Hindi, yaliua zaidi ya watu 230,000 kutoka mataifa 14 na kusababisha
kijana huyo kutengana kabisa na familia yake kwa muda.
Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo aliguswa mno na stori ya kijana Martunis na kuamua kukutana naye
Kwa sasa,
Martunis amejiunga na akademi maarufu ya klabu ya Sporting Lisbon ili
kutimiza malengo yake ya kuwa kama Cristiano Ronaldo, na Luis Figo
ambaye ameshastaafu.
'Nina
furaha kubwa kuwa hapa, klabu hii inanifanya niweze kufikia malengo
yangu,' alisema. 'Nina furaha kubwa sana kupata fursa hii. Viva
Sporting!
Martunis akiwa na rais wa FIFA Sepp Blatter
0 comments:
Post a Comment