Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Diaspora Initiative, Emmanuel Mwachullah (kulia) akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wamkutano wa wandishi wa habari uliofanyika MAELEZO jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Bw. Maggid Mjengwa mwanzilishi na mwendeshaji wa kipindi kipya cha televisheni, NYUMBANI NA DIASPORA akifuatiwa na Mkurugenzi wa Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Rosemary Jairo.
Na Andrew Chale, modewjiblog
Mwandishoi nguli na blog mwandamizi nchini, Maggid Mjengwa mapema leo amekitambulisha rasmi kipindi kipya cha televisheni kijulikanacho kama: ‘NYUMBANI NA DIASPORA!’, kitakachoanza kuruka kwa mara ya kwanza Ijumaa hii majira ya saa nne usiku ya Juni 26.2015 kupitia televisheni hiyo ya Taifa huku marudio yake yakitarajiwa kuwa Jumapili saa 10, jioni.
Akizungumza na wandishi wa habari, Ndugu Mjengwa ambaye pia aliongozana na vijana wake ‘Makamanda’, aliweza kupongeza ushirikiano uliopo nchini hasa kwa wanahabari na vijana kwa ujumla huku akitoa machache kuhusiana na ukumbi huo wa Idara habari Maelezo, Historia ambayo wengi wetu tulikuwa hatuifahamu.
Mjengwa aibainisha kuwa, wakati huo anapata elimu yake, miaka ya 80, aligusia kumbukumbu za ukumbi huo wa MAELEZO, Kwamba wakati nasoma Sekondari miaka hiyo, alikuwa na mazoea ya kwenda maktaba kuu, na kama duniani kulikuwa na habari kubwa, basi, mahali hapo, ambapo palikuwa ni American Information Centre, kulikuwa ikionyeshwa, kila saa saba mchana, matangazo ya TV kutoba CBS moja kwa moja kupitia satelite. Wakati huo yeye alikuwa nimmoja wa vijana wadogo waliokuwa wakifika mahala hapo kusikia mtazamo wa Wamarekani kuhusiana na suala ambalo wakati huo lilitikisa dunia.
Aidha, Mjengwa alibainisha kuwa, lengo la kipindi cha NYUMBANI NA DIASPORA ni kuonyesha yale ambayo watu wengi hawajayafahamu kuhusiana na dhana pana ya DIASPORA hasa kwa nyumbani Tanzania ambapo kipindi hicho kitakuwa kikielezea mambo mbalimbali ikiwemo kuwahoji watu waliokuwa wakiishi Ughaibuni na wengine waliopo nchini waliokuwa huko ughaibuni.
“Kwa kuanzia watu wasubiri kushuhudia mambo makubwa na muhimu ambayo hawakuwahi kupata kusikia. Kupitia kipindi hiki watayasikia na kuyaona. Pia tutashuhudia mahojiano ya Diaspora wa kwanza kabisa ambaye alikuwa ndio kijana pekee katika umri wa miaka zaidi ya 20, kuweza kupata uongozi wa juu nje ya Tanzania na baadae akaja kuwa gumzo Duniani kote” alieleza Mjengwa.
Pia Mjengwa alibainisha kuwa, watanzania zaidi ya milioni mbili, waliopo nje ya Tanzania wanaoishi Diaspora wanatakiwa kufikiwa hivyo kupitia NYUMBANI NA DIASPORA, itakuwa ni njia ya rahisi ya kuwafikia kwani anaamini kuwa kati ya watanzania 10, kati ya 8, wana ndugu nje ya nchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Rosemary Jairo alibainisha kuwa kupitia DIASPORA waliopo nje ndio daraja la kiuchumi wan chi yetu kwani kupitia wao, tutaweza kufika mbali kimaendeleo hasa kuwatumia kutokana na ujuzi walioupata huko nje wanakoishi.
Pia Bi. Rosemary Jairo alisema kupitia kitengo hicho cha Diaspora ndani ya Wizara, kimekuwa na fursa kwa kutoa ajira kwa watanzania Diaspora kwani wao ni asili na chimbuko la Tanzania hivyo ujuzi na maalifa yao yataendelea kusaidia nchi yao.
Aidha, alipongeza juhudi za Diaspora wa Tanzania kwa kuendelea kusaidia nchi katika mambo mbalimbali ambapo alifafanua kuwa, tayari madaktari kutoka mataifa mbalimbali wanatembelea Tanzania wakiretwa na Diaspora wa Tanzania waliopo nje ya Nchi.
“Kwa sasa manufaa ya Diaspora yanaendelea kuonekana, tayari tuna madaktari kutoka Marekani wapo Arusha wakiendelea na kutoa huduma mbalimbali. Na wengine wanatarajia kuja Nchini hivi karibuni ambao watakuwa katika Hospitali ya Mwananyamala na kwingineko…Hawa ni watanzania wenzetu ambao wanaguswa na nchi yao na sasa wanashirikiana na wataalam wengine kuja Tanzania kufanya mambo haya mazuri” alibainisha Bi. Rosemary Jairo.
0 comments:
Post a Comment