Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza, akitoa hotuba yake baada ya ufunguzi wa kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya nchi ya Comoro na Tanzania kwa wadau na wafanyabiashara kutoka Tanzania (hawapo pichani). Kongamano hilo limeanza tarehe 23 Aprili, 2015 likiwa na lengo la kufungua fursa mpya za biashara na uwekezaji nchini Tanzania na Comoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (mwenye suti ya bluu) Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb) wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Comoro Mhe.Ikililou Dhoinine (mwenye mavazi meupe) pamoja na viongozi, wafanyabiashara na wadau kutoka Sekta Binafsi baada ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya nchi ya Comoro na Tanzania lilioanza tarehe 23 Aprili, 2015.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe.
Mhandisi Christopher Chiza (Mb) amewaeleza wananchi wa Visiwa vya Comoro
pamoja na wafanyabiashara kuwa Serikali ya Tanzania imejithatiti katika
kuboresha wigo mpana katika masuala ya ili kuweza kukuza uchumi na
uwekezaji nchini.
Amesema
hayo akiwa anatoa Hotuba yake kwa Wadau na Wafanyabiashara
kutoka Tanzania baada ya ufunguzi wa Komango la Biashara kati ya Comoro
na Tanzania jana Alhamisi tarehe 23 Aprili, 2015.
"Miongoni
mwa maeneo ambayo Serikali ya Tanzania imeweza kuyaboresha
ili kurahisisha na kuongeza uwekezaji ni pamoja kujenga Miundombinu bora
yaani Barabara, kuboresha Viwanja vya Ndege, Bandari itarahishisha
uchukuzi na kuongeza fursa katika nchi SADC", alisema Waziri Chiza.
Chiza
aliongeza kuwa, mazingira ya kibishara kwa Tanzania yanalindwa na Sera
zilizopo kwa kupitia Sera ya Ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi
yaani (PPP) inalinda na kusimamia masuala ya uwekezaji baina Sekta ya
Umma na Sekta Binafsi.
Wafanyabiashara
kutoka nchini Tanzania wametaja baadhi ya changamoto zinazowakabili
ikiwa ni pamoja na pamoja na ushuru wa forodha kuwa mkubwa
visiwani Comoro, Usafiri usio wa uhakika unaosababisha bidhaa zao
kuharibika mara kwa mara pamoja na mahitaji ya viza kuingia na kutoka
nchi Comoro.
Mapema
wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Rais wa Visiwa vya Comoro
Ikililou Dhoinine amesema, "tayari ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje ya
nchi yake ishirikiane na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania kwa lengo la
kuondoa matumizi ya viza baina ya Tanzania na Comoro ili kuweza
kurahisha masuala ya biashara katika nchi hizi.
Waziri
Chiza alimalizia kwa kusema kuwa, Visiwa vya Comoro vina fursa nyingi
za uwekezaji na biashara ikiwemo huduma ya usafiri wa majini, anga pwani
zenye madhari kwa uwekezaji wa Hoteli za kimataifa, ambapo amewashauri
wawekezaji wa Tanzania kutumia fursa ya mkutano huo kuyabaini na
kuyafanyia kazi.
Imetolewa na Francisca Swai Afisa Habari
Ofisi ya Waziri Mkuu,
24 Aprili,2015
0 comments:
Post a Comment