Na Canal Mathias,
Ndugu zangu kwanza nawasalimu lakini pili nawapongeza katika utendaji kazi kuhakikisha taifa letu linasonga mbele zaidi.
Leo nimewiwa kuanza kwa kuuliza swali hivi mtu huzaliwa kuwa kiongozi ama hutengenezwa kuwa kiongozi? Nimeuliza hivi kwa kuwa nimeona viongozi wengi sana wakiongoza watu lakini watu wakitazama uongozwaji huo ni mithili ya wao kutofahamu kwanini wanaongozwa.
Everybody can be a leader but doesn't mean that can be responsible (Kila mtu anaweza kuwa kiongozi lakini sio kila kiongozi anaweza kuongoza)...Katika tafakuri yangu nimeona kwamba uongozi ni wa kila mtu, japo mtu huyo anaweza kuwa kiongozi na bado asiweze kuongoza kwa minajili ya kuamini kwamba uongozi ni kipaji kama ilivyo uimbaji mtu anaweza kuimba kwa kujifunza ama kwa kipaji chake binafsi.
Wakati mwingine viongozi walio wengi huanza kuonekana wakiwa wadogo sana wakiwaongoza wenzao ifahamike kuwa uongozi kiasili ni pale panapokuwa na watu zaidi ya wawili na kunahitajika kutoa maamuzi mmoja wapo atakuwa kipaombele katika hilo maana yake wengine kuwa wamekubali kuongozwa.
Mwandishi maarufu Stephen R. Covey katika kitabu chake cha "The 8th Habit From Effectiveness to Greatness" anaonekana kupingana na mawazo ya wengi kwa kuweka msimamo wake kuwa Viongozi hawazaliwi wala hawatengenezwi ila mazingira huwafundisha na kuwalea hiyo ndiyo sababu kubwa ya wao kuwa viongozi.
Kikawaida Asili na Asilia ni vitu viwili tofauti lakini nguvu ya Asili ya mwanadamu ni pamoja na kufanya chaguo, hivyo mwandishi Stephen alionyesha wazi kuwa kiongozi hujitengeneza kwa kuchagua mwenyewe.
Lakini Dkt Noel Tichy yeye alieleza wazi kwa mtazamo wake kuwa kiongozi hazaliwi bali hutengenezwa kwa kufundishwa maana yake ni kwamba watu hutumia nguvu yao ya kuchagua kujifunza na na kufuata mafunzo yanayoboresha mbinu ya uongozi.Kwa msemo huo kuna maana kuwa kila mtu anaweza kuwa kiongozi kwa kujitambua na kuamua kujifunza misingi ya uongozi bora na si bora kiongozi.
Ama hakika uongozi ni misingi na maono bora yenye hulka changanuzi kwa minajili ya upembuzi ulio yakinifu katika mtazamo wa hulka ya kipekee ya binadamu ambayo yaweza jenga taswira huru na chanya na ikiwa hasi basi hapo lipo jambo tororo lililonyemelezi ikiwa ni pamoja na tafakuri fupi kama ilivyo malengo duni anayojiwekea binadamu.
Ila asilimia kubwa ya viongozi waliofanikiwa katika uongozi wao wamepitia na kuwa na mambo kede wa kede ikiwa ni pamoja na taswira chanya.Tutazame tabia za kipekee na ambazo mara nyingi hufanana ambazo viongozi wanapaswa kuwa nazo;
1.KUWA NA MAONO (VISION). Pamoja na kuwa na hulka na mtazamo chanya lakini bado kiongozi anapaswa kuwa na maoni katika utendaji wake ama uongozi wake, Mwandishi aliyebobea nchini Marekani Warren Bennin alisema uongozi ni kubadilisha maono kuwa uhalisia..Hapa ndipo tutakapo fahamu uhalisi na uhalisia kama maneno yanayofanana lakini yana utofauti sana.
2.HUTENDA KWA KUFUATA DHAMIRA (CONSCIENCE). Unapokuwa kiongozi ni lazima kutenda kuwa na dhamiri yaani maono ya ndani ya nafsi ili kuweza kutofautisha jema na baya. Mwandishi Steven Covey katika moja ya maandishi yake aliwahi kusema "Sauti hii ya ndani ni tulivu na ya amani" Hapa alikuwa na maana kwamba maamuzi ya kushirikisha nafsi ni zaidi ya maamuzi ya kutojiridhisha yaani maamuzi ya hasira kwani hii ni dhamira inayotafsiri maono ya huruma kwa wengine sio tu kwa kuwa umekuwa kiongozi basi uishie kuburuza wengine kwa minajili ya cheo ulichonacho.
3.KUJITOA MUHANGA KWA AJILI YA WENGINE (RISK TAKER). Uongozi ni wito na kujitoa kwa ajili ya wengine, hivyo kiongozi bora ni yule anayekubali kujitoa ili kuhakikisha wengine wananufaika kupitia yeye kwa mtazamo chanya yaweza kuwa ni kufanikiwa kimaisha ama yaweza kuwa ni kufanikiwa kimtazamo.
4. KUWA NA SHAUKU KUBWA YA KUTENDA (PASSION). Mjasiriamali mwenye mafanikio na Mwandishi wa vitabu Antony Robbins anasema "There is no greatness without a passion to be great, whether its the aspiration of an athlete or an artist, a scientist, a parent, or a businessperson"
Naam, Kwani imani ipo wapi kati ya kuzaliwa ama kiongozi kutengenezwa misingi ipo mingi kwamba uongozi ni kipawa yaani kipaji lakini kisiwe na usaliti wa kufanya makubaliano na wenzako halafu ukipindua kichwa unawageuka wenzako. Maamuzi magumu yenye tija kwa wengine ni sawa tena yatakupa nguvu na heshima kubwa lakini sio maamuzi magumu yenye manufaa kwako pekee.
Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal
0756413465
Mzawa wa Iramba-Singida
0 comments:
Post a Comment