METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, April 24, 2015

AMKA MTANZANIA.!

 

By Malisa GJ & Makirita Amani,

Ni mara ngapi umewahi kuangalia watu ambao mmekua pamoja au mmesoma pamoja na kuona wao wamefanikiwa sana kwenye maisha kuliko wewe?

Unakutana na rafiki yako ambae mlipotezana miaka mitano au hata iliyopita. Katika kuzungumza kuhusu maisha anakwambia yeye ana kazi au biashara inayolipa sana, ana nyumba mbili, magari matatu na mashamba.

Ukijifikiria wewe huna kazi wala biashara ya kueleweka, bado unaishi kwenye chumba kimoja cha kupanga na usafiri wako ni daladala. Kiatu tangu ununue mwaka jana hujawahi kubadili. Hichohicho ndo ibadani, kwny harusi, msibani, kazini etc. Suruali unazo mbili unabadilisha pale unapopata mtoko.



Unajisikiaje baada ya kukutana na mwenzio mliyesoma nae na amefanikiwa kimaisha.?

Mbaya zaidi unakuta mtu huyo alikuwa hana uwezo sana darasani. Ulikuwa unafaulu zaidi yake. Unapata hasira na kujiona umeshapoteza maisha! Unajiona wewe si mwenye bahati. Unajiona huna future. Unajiona mwenye mikosi. Hiki ndicho kinachotokea kwa watu wengi.

UFANYE NINI?

Ktk maisha yako usijaribu kujilinganisha na mtu mwingine. Kila mtu ana nafasi yake ktk maisha ya kumuwezesha kufanikiwa. Kama si leo basi kesho.

Kama wewe kila siku ni kujilinganisha na wengine, kosa hili ni baya sana na litakugharimu sana kwenye maisha yako. Unaweza kusema kujilinganisha na wengine kunakupa wivu wa maendeleo au kunakufanya ukazane zaidi, huo sio ukweli hata kidogo.

Kujilinganisha na wengine na hasa pale wanapokuwa wamefanikiwa kushinda wewe ndio unazidi kujirudisha nyuma. Unajisikia vibaya sana kuona mtu uliyemfundisha kusoma na kuandika mlipokuwa shule ya msingi, unamfuta makamasi eti leo anatembelea "Ford Explorer" wewe huna hata baiskeli. Hapa ndipo unapoanza kuona labda wewe una kisirani na yeye ana bahati au kuanza kuhisi alibebwa.

Hapana. Usiwaze hivyo. Kila mtu ni wa pekee. Dunia ina watu zaidi ya bilioni saba, lakini kati ya watu hao hakuna hata mmoja anayefanana na mwenzie. Hata mapacha hawana ufanano wa asilimia 100.

Wewe ni wa pekee, una uwezo mkubwa na vipaji vya kipekee. Hakuna mtu yeyote duniani anayeweza kufanya vitu fulani kama unavyoweza kufanya wewe. Tatizo ni kwamba hujaweza kujua ni jinsi gani utumie vipaji vya pekee ulivyonavyo ili kutimiza ndoto zako.

Ni muhimu kuelewa kuwa duniani hatupo sawa hivyo hatuwezi kufanikiwa kwa usawa. Wewe ni wa pekee (unique) na una vitu unique ambavyo unaweza kuvitumia kupata mafanikio. Unahitaji tu kushikwa mkono ujue potentials ulizonazo na uweze kufanikiwa.

We unadhani Jotti hakupenda kusoma? Hakupenda kuwa na "digrii" au "mastazi" kama wewe? Hakupenda siku moja nae aitwe "Dokta Joti?". Sasa kwanini hakusoma?

Ni kwa sababu elimu kwake haikuwa one of his unique potetials. Yeye alijua potential yake ipo kwenye "comedy" do akawekeza nguvu na akili yake yote kwenye "comedy" na hatimaye amefanikiwa.

Je wewe umejua potential yako iko wapi? Kama hujui huwezi kufanikiwa. Unaforce utangazaji kumbe your potential ipo kwenye ufundi magari. Unaforce kusomea sheria ili na wewe uitwe "advocate" kumbe potential yako ipo kwenye ualimu.

Matokeo yake unakuwa mtangazaji, au mwanasheria usiye na mvuto. Miaka kumi Hufanikiwi. Kwa sababu umefanya kitu ambacho si potential yako.

Kuna mtu ana kipaji cha ualimu. Akikufundisha unaelewa kuliko mwalimu mwenye uzoefu. Anachohitaji ni kwenda kusomea taaluma tu ya ualimu aweze kuserve potential yake. Lakini ukimuuliza anasema "siwezi kusoma ualimu kazi ya Ajabu. Naenda kusoma Sociology"

Anamaliza Sociology anakaa miaka mitano bila kazi. Anatafuta hata mahali pa kuvolunteer hapati. Ni kwa sababu aliserve potential isiyo yake.

Kuna wengine wanaishi kwa kukariri. Ameona umesomea sheria ukafanikiwa, naye anataka akasome sheria eti awe kama wewe. Ameona umesomea uhasibu nae anasema "nataka kusoma uhasibu niwe kama fulani". Acha mawazo potofu. Nani alikuambia maisha yana formular? Usisafirie nyota ya mwenzio. Kila mtu anasafiri kwenye njia yake binafsi.

Kama potential yako ni ualimu, somea ualimu kisha fanya kwa bidii utafanikiwa. Mbona wako walimu wanatembelea "Vorgue" na kuna wahasibu, wanasheria au wengine wanaosomea taaluma zinazoonekana zina hela lakini hawana hata na baiskeli.

Jitambue na jiamini. Tambua potential yako na uanze kuifanyia kazi mapema. Mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide alisomea degree ya kwanza ya uchumi. Alipomaliza akaajiriwa bank. Lakini akaona kukaa bank si potential yake. Akaamua kufanya mziki ambao ndio ilikua potentia yake.

Akaanza kuimba na amepata mafanikio kupitia sanaa ya muziki. Baadae akarudi chuoni akasomea "masters" ya uchumi ili aweze kufanya kazi yake ya muziki vizuri. Na amefanikiwa sn. Lakini kama Koffi angeendelea kufanya bank pengine angeishia kuwa "bank teller" nothing more.!

Sasa wewe unajua potential yako ipo kwenye kucheza soka lakini unalazimisha shule. Unaishia kufeli. Umefeli form four lakini hukubali unarisiti mara tatu. Baadae unapata "credit" na kwenda form five. Unajilazimisha kukariri na inafika chuo kikuu.

Unafurahi kuwa sasa na wewe ni mwanachuo. Unasomea degree ya Marketing. Hujui hata Marketing ni kitu gani lakini unaforce kisa umesikia watu wakisema "Marketing ina hela balaa"

Unamaliza na kuishia kutembea na vyeti juani miaka mitano. Wenzio uliokuwa ukicheza nao soka wapo TP Mazembe au timu nyingine kubwa na wanafanya vzr. Wewe uling'ang'ania "digrii". Nani alikuambia "digrii" ndio njia ya mafanikio? Muulize Wyne Rooney wa Manchester kama ana digrii au hata diploma? Acha kukariri maisha.!

Kila mtu anasafiri kwenye njia yake binafsi. Kuna ambao watafanya kazi na kufanikiwa sana, kuna ambao watafanya biashara na kufanikiwa mno. Pia kuna wengine watatumia vipaji vyao na kufanikiwa pia.

Muhimu ni kujua njia yako ya kufanikiwa ni ipi. Unapojaribu kujilinganisha na watu ambao wako kwenye njia tofauti hujitendei haki wewe mwenyewe.

Kama hujafanikiwa kama wenzako walivyofanikiwa huenda hujajua ni kitu gani unachofanya kwenye maisha yako. Huenda hujajua ni kitu gani cha kipekee unachoweza kufanya na ukafanikiwa sana. Na kwa asilimia kubwa huenda unaiga maisha ya watu wengine.

Usipende kujilinganisha na mtu. Jilinganishe na wewe mwenyewe. Tumia mfano wa Christian Bella aliulizwa na waandishi wa habari anapenda kuwa kama nani. Akajibu "napenda kuwa kama Christian Bella". Hii ni kwa sababu anajikubali. Na hii imemsaidia kufanikiwa sn kwny muziki wake.

Lakini wewe kila siku ni kujilinganisha na wengine. Eti fulani alimaliza chuo akaenda kugombea ubunge akashinda, na mimi nikimaliza chuo naenda kugombea ubunge kule kwetu. Acha ujinga. Utapata kura yako na ya girlfriend wako tu. Kama potential yako ipo kwenye biashara kwanini unalazimisha kufanya siasa?
Siri ya mafanikio ni kutambua "potential" yako na kuanza kuitumia kupata mafanikio but pia kujiamini wewe mwenyewe. Kuanzia leo anza kujilinganisha na wewe mwenyewe. Usijilinganishe na mtu.

Jiulize hicho unachofanya kwenye maisha yako je unakifurahia? Kumbuka ni vigumu sana kufanikiwa kama unafanya kitu ambacho hukipendi. Jiulize ni vipaji gani ulivyonavyo, jua ya kwamba una uwezo mkubwa na ubunifu wa hali ya juu. Vijue na kutumia vitu hivi ili kuboresha maisha yako.

Shindana na wewe mwenyewe. hakikisha kila siku mpya unakuwa bora zaidi ya siku iliyopita. Unapomaliza siku ya leo hakikisha umefanya vitu unavyofanya kwa ubora zaidi ya ulivyofanya jana. Kwa njia hii utajikuta ufanisi wako unaongezeka kila siku na mwishowe unapata mafanikio makubwa.

Kama unafanya vitu kwa mazoea tayari upo nje ya njia ya kuelekea kwenye mafanikio. Kama sababu pekee inayokufanya uende kwenye shughuli zako leo ni kwa sababu jana ulienda upo kwenye hatari kubwa.

Hakikisha kila siku una kitu cha kuongeza kwenye ujuzi na ufanisi wako wa kazi. Hakikisha kila siku kuna kitu kipya unajifunza ambacho kitakusaidia kwenye maisha yako. Tambua "potential" zako na uzitumie.

AMKA MTANZANIA.!
Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!
Credits kwa Makirita Amani ambaye ameandika sehemu kubwa ya makala hii nami nikongezea tu.! Kwa makala nyingine nzuri kuhusu maisha tembelea www.amkamtanzania.com/?m=1
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com