METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, November 29, 2023

PROFESA NDALICHAKO- MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KULETA FAO JIPYA LA HUDUMA YA MTENGAMAO


Na Mwandishi Wetu; Dar es salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa mifuko inayowezesha wafanyakazi na kupitia mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) inatarajia kuanzisha fao jipya la huduma ya mtengamao.

Ameyasema hay oleo tarehe 29 Novemba, 2023 alipo kutana na kufanya mazungumzo na wanufaika wa mfuko huo na kusema kwamba fao hilo linatarajiwa kuanzisha Elimu ya Ufundi Stadi kwa Wafanyakazi waliopata Ulemavu kazini, litasaidia kubadilisha mazingira ya nyumba kwa kulingana na Ulemavu ulionao.

Aidha Waziri Ndalichako ameishukuru serikali ya awamu ya sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hatua alizozichukua kuweka riba nafuu kutoka asilimia 10 mpaka asilimia 2 kwa mwezi ili kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji.

Kwa niaba ya wanufaika wa Mfuko huo ameishukuru Serikali kwa huduma wanazopokea kutoka katika Mfuko huo licha ya kupata ulemavu na wengine kuondokewa na wapendwa wao.

“Naomba kuhamasisha waajiri kuweza kuwachangia wafanyakazi wao, kwani viwango vya uchangiaji ni vidogo tunaishukuru Serikali imepunguza viwango vya uchangiaji hadi kufikia asilimia 0.5” Alisema Norbert Tesha,
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com