METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, September 16, 2023

ALHAJ KIMBISA AWAGEUKIA WAKUU WA WILAYA WA MKOA WA DODOMA KWENDA SAMBAMBA NA DHAMIRA YA RAIS SAMIA


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mkoa wa Dodoma Alhaj Adam Kimbisa amewahimiza wakuu wa wilaya wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo wa kuhudumia mwananchi ili kutekeleza Ilani ya CCM na hivyo kwenda sambamba na dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Kimbisa ametoa rai hiyo leo Jijini Dodoma alipokutana na viongozi hao kwa nia ya kujitambulisha, kuzungumza nao na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwahudumia wananchi kikao ambacho kimehudhuriwa pia na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC),Donald Mejitii na kwa upande wa serikali kimehudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemarry Senyamule.

 “Mimi hapa sijawaita kwa sababu ya Chama,nimewaita kwa sababu ya wananchi,na kubwa lililonifanya niwaite ni kwamba nimekuja kujisalimisha kwenu,maana tangu nimechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Novemba 21 mwaka jana hatujapata nafasi ya kuzungumza pamoja kuhusu hatma ya wananchi wa wetu katika kuwafikishia huduma,

 “Sasa tutamuhudumia vizuri mwananchi kama wote tukijua wajibu wetu,mimi Chama,wewe Serikali na wengine kwa Halmashauri muhimu ni kuhakikisha huduma anazostahili mwananchi azipate vizuri na kwa wakati bila ya kujali nani anawapa, hivyo kama sisi nguvu zetu zote zinatokana na wananchi ni vyema tujadili nak uangalia ni jinsi gani wananchi watapata huduma kupitia uongozi wetu,”amesema Kimbisa.

Awali akitoa neno la utangulizi Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbanga amesema kikao hicho ni muendelezo wa vikao vya Mwenyekiti vya kukutana na makundi mbalimbali tangu achaguliwe lengo likiwa ni kuweka mikakati ya pamoja ya kuwahudumia wananchi.

Mkoa wa Dodoma una wilaya saba ambazo ni Dodoma, Bahi, Chamwino, Mpwapwa, Kondoa, Chemba na Kongwa.

Mwisho
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com