METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, August 16, 2023

IKUNGI YASIMAMA KWA MUDA//MBUNGE MTATURU AWATAKA WANANCHI KUTHAMINI MIRADI YA MAENDELEO

Wananchi wametakiwa kuthamini miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na kuachana na upepo wa kisiasa unaoweza kuwaondoa kwenye msitari wa kupata maendeleo. 

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu wakati akiongea na wananchi wa Kata ya Ikungi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika stendi mpya ya mabasi Ikungi.

Mhe.Mtaturu amesema kumekuwa na upotoshwaji kuhusu uwekezaji hasa katika sekta ya bandari ambao umekuwa ukipigiwa kelele hivi karibuni na ambapo amesisitiza kwa kusema hakuna kinachouzwa bali ni uwekezaji ambao utasaidia kuongeza pato kwa taifa na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi ikiwemo mikopo isiyoumiza,Elimu,Afya,Maji na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Katika kusisitiza hilo amekemea wanasiasa wanaomtukana Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumkashfu kuwa ameuza nchi “Unaenda kumtukana mama ambaye ulisema umekimbia mama akakutafuta huko Ubeligiji akakwambia njoo nyumbani ukamwambia ninamadai yangu akalipwa akaja akasema mama amefungua Nchi siku mbili unaanza kumtukana umelogwa au umenunuliwa wewe?”

Hata hivyo Mhe. Mtaturu amewaomba wananchi wa Singida Mashariki kuendelea kuunga mkono juhudi na maendeleo yanayoletwa na serikali ya awamu ya sita ambayo kwa kipindi cha miaka miwili amefanya mageuzi makubwa yakimaendeleo.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com