METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, May 10, 2023

SERIKALI KUBORESHA MTANDAO WA MAWASILIANO MISENYI



Na Mathias Canal, Dodoma

 

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imetekeleza miradi ya mawasiliano iliyokamilika katika kata 10 za Wilaya ya Missenyi.

Kufikia mwezi Machi, 2023 tayari ujenzi wa minara 13 imekamilika na inatoa huduma katika teknolojia ya 2G na 3G.

 

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Mhandisi Mathew Kundo ameyasema hayo leo tarehe 10 Mei 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe Frolent Laurent aliyetaka kyfahamu lini serikali itaongeza minara au kuboresha mawasiliano katika kata zote 20 za Wilaya ya Misenyi?

 

Mhandisi Kundo amesema kuwa kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali Serikali imeshapata watoa huduma wa kufikisha huduma za mawasilioano katika Kata za Bugorora, Kasambya, Mutukula na Kakunyu ambapo tayari zimeshapata watoa huduma.

 

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com