Na Saida Issa,Dodoma
MBUNGE wa Kishapu Boniface Butondo amtaka Waziri wa habari, mawasiliano na Teknolojia ya habari kusimamia wamiliki wa vyombo vya habari nchini kutoa mikataba kwa waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi Kwa weledi.
Mbunge huyo ameeleza hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo amesema kuwa Waziri Nape anatakiwa Kulinda maslahi ya waandishi wa habari ili wafanye kazi kama watumishi wengine.
"Waandishi wa habari wanapitia magumu sana katika majukumu yao naongea kwa masikitiko sababu wengi wao hawana mikataba ya kazi hiyo inawafanya wafanye kazi katika mazingira magumu sana,"amesema
Amesema kuwa Serikali kupitia wizara ya habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari wanalojukumu la Kulinda,kusimamia na inawezekana waandishi kupatiwa mikataba kama Serikali itasimamia suala hilo.
0 comments:
Post a Comment