MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amegawa mitungi ya gesi 700 kwa wanawake wajasiriamali 700 wa Mkoa wa Mwanza lengo ikiwa ni kuhamasisha kuacha matumizi ya nishati chafu ( kuni na mkaa) na badala yake watumie nishati safi ili kuhifadhi mazingira na pia amekabidhi fedha kiasi cha shillingi milioni 21.
Hafla hiyo imefanyika leo Machi 27, 2023
katika Ukumbi wa Rocky City Mall jijini Mwanza, ambapo mgeni rasmi alikuwa
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Ndugu Reuben Sixbert Jichabu
Akizungumza katika hafla hiyo, baada ya
kukabidhi majiko kwa niaba ya Mhe. Masanja Bw. Jichabu amewataka wanawake hao
kutumia nishati ya gesi ya ORYX katika shughuli zao za ujasiriamali na kuepuka
matumizi ya kuni.
Naye, Mhe.
Masanja aliahidi kuendelea kuwaunga mkono wajasiriamali wanawake wa Mkoa wa
Mwanza ili waweze kukuza uchumi wao.
Aidha Katika
Hatua nyingine Mbunge Marry Masanja alizishukuru Kampuni za ORYX na FOMAC kwa
kudhamini na kufanikisha tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment