METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, February 22, 2023

TANESCO IMEJIPANGA KUFIKIA MEGAWATI 5000 IFIKAPO 2025


Na Saida Issa, Dodoma

KATIKA kutatua changamoto ya upatikanaji wa umeme nakupelekea mgao wa umeme shirika la umeme tanzania tanesco limesema kuwa kwa sasa hali ya upatikanaji umeme imeimarika tofauti na ilivyokuwa mwaka 2022 ambapo uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini ni Megawati 1,820, kwa sasa mitambo iliyopo inazalisha Megawati 1,300.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shirika hilo kaimu mkurugenzi huduma kwa wateja shirika la umeme tanesco Martin Mwambene alisema serikali imeendelea na ujenzi wa miradi mbalimbali itakayoongeza kiwango cha uzalishaji nakuondoa adha ya wananchi kukosa huduma.

"TANESCO inafanya miradi kadhaa ambayo inasaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka ambapo malengo ni kufikia Megawati 5,000 ifikapo mwaka 2025,"alisema.

Aidha alisema kuwa Mradi wa Umeme wa bwawa la Julius Nyerere upo asilimia 88 ambapo sasa hivi tumeanza kujaza maji ambayo kwa sasa yamefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari.

"TANESCO ina miradi mbadala ambayo itaongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme ikiwemo ya gesi na jua, pia kuna vyanzo binafsi vyenye uwezo wa kuzalisha umeme mfano viwanda vya sukari,

Miradi ya uzalishaji umeme inaenda sambamba na miradi ya kusafirisha umeme, katika mradi wa JNHPP kuna njia ya kusafirisha umeme itakayoanzia Rufiji mpaka Chalinze na tayari transfoma kubwa takriban sita zimepelekwa zinasubiri kufungwa,"alisema.

Kadhalika alisema Kuna baadhi ya mikoa ikiwemo Rukwa na Katavi haipo katika Gridi ya Taifa, hivyo kuna laini ambazo zitajengwa ambazo zitakuwa zinaunganisha nchi na nchi nyingine,Karibu nchi nzima itakuwa ipo katika mfumo wa Gridi ya Taifa.

Mradi wa Gridi Imara utajumuisha ununuzi wa mashine umba 6,000, mita laki 7 za umeme, nguzo 380,000, ununuzi na ufungaji wa nyaya zenye urefu wa KM 40,000, ujenzi wa vituo 14 vya kupoza umeme na ujenzi wa njia za kusafirisha umeme mkubwa takriban KM 948.

Mradi huu wa Gridi Imara ni ushahidi kwamba matatizo ya umeme yaliyopo nchini tunayafahamu na tunatarajia mradi huu utayatatua.

TANESCO haiuzi nguzo bali inauza huduma ya umeme,Aidha, inapothibitika kuwa nyumba iliyoungua imesababishwa na umeme, fidia huwa zinalipwa.

Kwaupande wake msemaji mkuu wa serikali na mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Gerson Msigwa amesema nishati ya umeme ni muhimu nanihitaji la msingi na lazima kwakila mtu ndio maana serikali inahakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wote popote walipo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com