Mamlaka ya
kusimamia uvuvi wa bahari kuu nchini ina
mpango wa kujenga kiwanda cha kuchakata samaki ambacho kitasaidia kuongeza
ajira kwa watanzania pamoja na kuendela kusimamia na kuratibu shughuli za uvuvi
katika bahari kuu.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dodoma Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kusimamia uvuvi
wa bahari kuu Dkt. Emmanuel Sweke amewataka wavuvi kulinda mazingira ya bahari kwa kuacha
matumizi ya uvuvi haramu.
Aidha Katika
hatua nyingine Dkt. Sweke amesema gharama
za leseni kwa wavuvi wa ndani ya nchi ni nafuu tofauti na wavuvi wa nje ya nchi katika bahari kuu ili kuhamasisha
watanzania kuchangamkia fursa za uvuvi katika bahari kuu.
‘’Mamlaka ya
kusimamia uvuvi wa bahari kuu ndio mamlaka inayohusika na utoaji wa leseni ya uvuvi katika pande zote mbili ambazo ni
Tanzania bara pamoja visiwani’’.
‘’Pia
Taasisi hii inajishughulisha na kuratibu
shughuli zote za uvuvi katika bahari ambapo makao makuu ya taasisi hiyo
yapo Zanzibar,’’amesema sweke.
Hata hivyo
alimalizia kwa kusema kuwa pindi kiwanda cha kuchakata samaki kitakapojengwa mkoani Tanga kitakuwa na uwezo
wa kuchakata tani mia moja hadi mia mbili za samaki kwa siku ambapo kiwanda hicho kitaweza kutoa ajira kwa watanzania mia
moja.
Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu ni Taasisi ya muungano yenye jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli zinazohusiana na uvuvi wa bahari kuu ikiwemo utoaji wa leseni za uvuvi pamoja na kuhakikisha mazingira ya bahari yanalindwa vizuri.
0 comments:
Post a Comment