METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, February 8, 2023

MHANDISI MMASSY AWAASA WANANCHI KUTOCHIMBA VISIMA VYA MAJI KIHOLELA

21-860x573

MKURUGENZI Bodi ya Maji,Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa fupi ya Utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo jijini Dodoma.

Na Rahma hajia, Na Getrude Vangayena Dodoma.

Bodi ya maji bonde la Wami Ruvu imewaasa wanachi kuacha uchimbaji holela wa visima na kufuata taratibu zote zinazo takiwa kufuatwa  katika uchimbaji wa visima ili kuendelea kutunza vyanzo vya maji vilivyopo kwa matumizi ya  kizazi cha sasa na baadaye.

Akizungumza na  wanahabari jijini Dodoma wakati  akileza utekelezaji wa majukumu ya bodi ya maji bonde la Wami/Ruvu  Mkurugenzi bodi ya maji bonde la Wami Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy amewaasa wananchi kufuata sheria zan uchimbaji wa visima.

Amesema bodi hiyo haijafata utawala katika kugawanya mto Ruvu  ila imefata namna mto ulivyogawanyika ,mto Ruvu umeanzia katika safu za milima ya uluguru iliyopo mkoani  Morogoro na kuishia katika bahari ya Hindi.

‘’ mto wami Ruvu hujafata mgawanyo wa utawala umeanzia milima ya uluguru, wilaya Ya mpwapwa ,chenene Dodoma na makutupora Dodoma’’

Lakini pia  Amesema kuwa majumu bodi ya maji  mto Ruvu ni kusimamia maji yaliyopo juu na ardhini ambayo yanajumuisha maji ya chemichemi,mabwawa, visima pamoja na maji ya chini ya ardhi ambayo inajumuisha bahari.

 ‘’Rasilimali za maji ni haki ya kila mtanzania ,kila mtanzania anatakiwa kupata maji hayo’’.

‘’ ili kila mtanzania  kufikiwa na  rasilimali hiyo ya maji serekali imeamua kuweka utaratibu ambao utawasaidia wananchi kupata maji hayo kwa kuanzisha Taasisi  ambazo chini ya wizara ya maji ,mtu anapotaka kutumia maji  kwa matumizi yoyote yale lazima afate taratibu za kutumia’’ amesema Mmassy.

Pia aliongezea kwa kusema kuwa  kuna   wadau mbalimbali ambao wana tumia maji hayo ambapo mdau wa kwanza ni mamlaka za maji nchini ikihusisha mikoa ya Dodoma,Dar es salaam,morogoro. 

Mhandisi Mmassy amesema bodi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  wananchi kufanya shughuli za kilimo maeneo ya jirani na vyanzo vya maji hali inayopelekea kuharibu vyanzo hivyo vya maji.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com