Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo katika mgodi wa Nyakafulu uliopo katika Kijiji na Kata ya Nyakafulu Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita, tarehe 9 Mei 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe Martha Mkupasi akizungumza na wachimbaji wadogo katika Wilaya hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko wilayani hapo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita Alhaji Said Maneno Kalidushiakizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyakafulu akielezea kiasi ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2020/2025 ilivyotekelezwa katika Wilaya ya Mbogwe mkoani humo, tarehe 9 Mei 2021.
Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo katika mgodi wa Nyakafulu uliopo katika Kijiji na Kata ya Nyakafulu Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita, tarehe 9 Mei 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel Robert akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi-Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko kuzungumza na wachimbaji wadogo katika mgodi wa Nyakafulu uliopo katika Kijiji na Kata ya Nyakafulu Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita, tarehe 9 Mei 2021.
Sehemu ya wachimabji wadogo waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko wakati akizungumza na wachimbaji wadogo katika mgodi wa Nyakafulu uliopo katika Kijiji na Kata ya Nyakafulu Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita, tarehe 9 Mei 2021.
Na Mathias Canal, WazoHuru-Geita
Serikali imesema kuwa haitosita kuyafuta machimbo yoyote yenye migogoro nchini ili kunusuru kadhia za migogoro na kuchukiana zinazoweza kuwakumba wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kusitisha leseni za uchimbaji.
Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko ameyasema hayo tarehe 9 Mei 2021 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo katika mgodi wa Nyakafulu uliopo katika Kijiji na Kata ya Nyakafulu Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita, tarehe 9 Mei 2021.
Amesema kuwa lengo la kufunga maeneo yote yenye migogoro ni kutoa nafasi kwa wahusika kuelewana wao kwa wao pamoja na serikali ya kijiji na serikali kuu.
“Nilikwenda Chunya nikafunga mgodi, nikaenda Mangae mkoani Morogoro nikafunga lakini walioanza kulia njaa ni wachimbaji wenyewe. Hivyo nawashauri toeni nafasi kwa mbunge wenu na serikali ifanye kazi ya maendeleo na sio kazi ya kutatua migogoro” Amesisitiza Waziri Biteko
Waziri Biteko amesema kuwa endapo mgogoro kati ya wachimbaji na wenye mashamba katika eneo la mgodi huo utamalizika, serikali ipo tayari kutoa leseni kwa ajili ya uchimbaji wa madini utakaosaidia wananchi kujipatia kipato na kulipa kodi ya serikali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel ameridhia ombi la Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Mhe Henry Maganga la kuwasamehe walioiba nyaraka na kuiba mashamba ikiwa ni pamoja na kuchochea migogoro katika eneo hilo la machimbo.
Mhandisi Gabriel amewasamehe wananchi hao huku akiahidi kuendelea kuwafuatilia mienendo yao.
Awali akisoma risala ya wachimbaji wadogo Katibu wa chama cha Wachimbaji wadogo (ISANJABADUGU) Steven Mosses amesema kuwa kikundi hicho kimeundwa kwa mujibu wa ilani ya CCM na sera ya Nchi kikihusisha wachimbaji wadogo wa Wilaya ya Mbogwe, Chato, Bukombe na Geita mji.
Amesema kuwa tangu kuanza kwa shughuli za uchimbaji wananchi 3600 wamenufaika na mgodi huo katika nyanja mbalimbali ikiwemo mama Lishe, nyumba za kulala wageni, Mabanda ya biashara, na uchenjuaji wa madini ya dhahabu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment