Na Hamis Hussein - Singida
Vyama
vya Mpira wa Miguu vya Wilaya Mkoani Singida vimetakiwa kusimamia Sera ya
michezo ya kuendesha mashindano mbalimbali katika maeneo yao ili kukuza vipaji
kwa vijana kuanzia ngazi ya Wilaya huku msisitizo ukiwa katika soka la
wananwake.
Afisa
Michezo wa Mkoa wa Singida Amani Mwaipaja Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa
Chama cha Soka cha Mkoa wa Singida SIREFA ambao umefanyika Jana Desemba
31 2022 katika Chuo cha Maendeo ya Wananchi FDC uanzishwaji na usimamizi wa
michezo katika maeneo husika huku
Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Mkoani Hapa Yagi Kiaratu akitilia mkazo Suala hilo.
“Kwenye vyama vya wilaya tuongeze nguvu katika kufanya mashindano, tunaweza tukawa tunaandaa mshindano kulingana na Geografia zetu mfano watu wa Iramba kuna center kama Kiomboi, Shelui na Ulemo tunaweza tumia center hizo tukapata timu zinazoweza kushiriki ligi ya wilaya hadi ya Mkoa”, Alisema Mwaipaja.
Alisema
Serikali kupitia kwa Waziri imeendelea kusisitiza mashindano mbalimbali
kufanyika ngazi ya chini lengo likiwa ni kuibua vipaji kuanzia umri mdogo ambao
watoto wanapokuwa shule wakijengewa misingi bora ya kushiriki michezo mbalimbali
hasa Soka.
Sanjari
na Hayo Afisa huyo wa michezo Mwaipaja alisisitiza kuwa ofisi yake itaendelea
kushirikiana na vyama vya soka mkoani hapa ili kuleta mabadiliko ya soka.
Mwenyekiti wa chama cha Soka la Wanawake Mkoani Singida Yagi Kiaratu alisema kuwa kwa sasa Mkoa wa Singida Umekuwa ukitolewa mfano katika uendeshaji ligi ya wananwake mkoani hapa hivyo alivitaka vyama vya soka ngazi ya wilaya kuekeza nguvu Zaidi ili kuibua vipaji kupitia soka la wanawake.
Mgeni
Rasmi katika Mkutano huo wa SIREFA Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TFF kanda ya
Kati Mohemed Aden ameahidi Kuwezesha Mafunzo ya Makocha mkoani Singida Ngazi ya
Awali na kutoa wito walimu wa shule za msingi kujitokeza kushiriki kozi hiyo
Aden
Alisema kuwa Makocha wengi wanaofundisha watoto bado wa elimu iliyopitwa na
wakati hivyo akahidi kuleta kozi hiyo kuhu akitoa kipaumbele kwa walimu wa
shule za msingi kusoma kozi hiyo kwani wao ndio wanaoanza kuajenga watoto
wakiwa wadogo shuleni.
“Nimeongea na Mwenyekiti
amsema makocha wengi elimu ambayo kwa sasa kama imepitwa na wakati hivyo
nitaangalia uhitaji wa walimu na nitaleta kozi ya Grass root (Kozi ya ukocha ya
Awali) kwa gharama zangu mimi mwenyewe”, Alisema Aden
“Na nitoe wito tu kwa
walimu wa shule za msingi wajitokeze kwa wingi kusoma kozi hiyo pindi
itakapotangazwa na SIREFA ili wapate kuwasaidi watoto kwa sababu watoto
wamekuwa wakiumia na ndoto zao za kucheza zinaishia njiani”, Aliongeza Mjumbe huyo wa kamati Tendaji
ya Tff
Kuhusu
Suala ya idadi ya Mashindano likatiliwa mkazo na Mwenyekiti wa chama cha soka
mkoani Singida SIREFA Hamis Kitila ambaye alivita vyama vya Soka vya Wilaya
Kuongeza idadi ya hasa kuanzia mwaka mpya wa 2023 na kusema kuwa mashindano
kuwa na timu chache katika eneo husika haitakubalika kulingana na taratibu zao.
Hamis
Alisema SIREFA kwa kushirikiana na Ofisi ya Ofisa Michezo wataunda kamati za
wilaya zitazokuwa zinafuatilia kutambua mashindo yote yanayofanyika yasiyorasmi
na yaliyo rasmi ili kuleta mabadiliko katika soka.
“ Hili Suala ya timu Sita
katika Mashindano halitakubalika, sisi singida mashindano kuwa yana timu 24
sasa sasa timu chache halitavumilika, na
tunampango wa kuwa na barua kwa
kushirikiana na afisa michezo kuyatambua mashindano yote yaliyorasmi na
yasiorasmi hivyo tutaunda kamati zitakazo simamia hilo”, Alisema Kitila.
Akizungumza
kwa Niaba ya wajumbe wa mkutano huyo wa SIREFA Mwenyekiti wa chama cha Soka
Wilaya ya Manyoni Rajabu Mlosha ameiomba Sekretarieti ya SIREFA kupunguza kwa
ada ya kiingilio cha Ligi ya Mkoa ili kuongeza idadi ya timu shiriki kwa kiasi
cha Shilingi 300000/ ni kikubwa
ulinganisha na mapato ya vilabu vinavyotaka kushiriki ligi ya Mkoa.
Katika
hatua nyingine Mkutano huo wa SIREFA
ulitoa taarifa ya mikakati ya kujenge Uwanja wa Kisasa wa kufanyia
Mazoezi ambayo eneo lenye ukubwa wa Ekari 4 limepatika Mtaa wa Manga na tayari
mchakato wa kujenga uwanja huyo zimeanza jambo ambalo wananchama wa
SIREFA limewafurahisha.
Mkutano
Mkuu wa SIREFA umefanyika jana Desemba 31 2022 katika chuo cha Maendeleo ya
Wananchi FDC Ikishirikisha wanachama kama Chama cha Soka Wilaya ya Singida
Mjini SIDIFA, Chama cha Soka Wilaya ya Manyoni (MADIFA), Chama cha soka Wilaya
ya Iramba (IRADIFA) , chama cha waamuzi (FRAT) chama cha Makocha TAFCA, chama
cha soka la wanawake Mkoani Singida TWFA, Sekretarieti na Kamati Tendaji ya
SIREFA.
0 comments:
Post a Comment