METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 29, 2022

REA YAZINDUA MRADI MPYA WA UMEME SINGIDA KUNUFAISHA WATU 1802

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Paskasi Muragili akizindua mradi mpya wa awamu ya tatu wa Kusambaza umeme
Vijiji miji Mkoani Singida mapema hii leo.

Wawakilishi wa Mkandarasi Central Electicals international limited wakikabidhiana nyaraka kwa ajili ya mradi wa kusambaza umeme 
vijijini mkoa wa singida.

Kaimu Mkurugenzi wa REA Nicolaus Moshi akiwa na Mwakilishi wa Mbunge wa Singida mjini Moses Ikaku na Mwakalishi wa Mkandarasi wa Kusambaza Umeme Vijijini Central Electicals International Limited wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya kufanya mazungumzo wa mradi mpya wa kusambaza umeme vijijini mkoani Singida.

Kikao kikiendelea 

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Paskasi Muragili akizungumza katika uzinduzi huo.

Kaimu Mkurungenzi wa Mipango na utafiti kutoka REA Nicolaus Moshi akitoa taarifa ya mradi.

Baadhi ya wafanyakazi wanaosambaza umeme wakiwa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa mradi huo.

Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu akitoa amelezo kuhusu ukosefu wa umeme wa wananchi wa vijiji vilivyopembezoni mwa mji.

Mwakilishi wa Mbunge wa Singida Mjini Moses Ikaku ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kisaki akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Na Hamis Hussein – Singida

Wakala wa Nishati Vijijini REA umezindua mradi  kusambaza umeme katika maeneo ya   vijiji  Miji katika  mkoani Singida  ambapo utatekelezwa kwa kujengwa Kilometa 40.5 za Msongo wa kati na msongo mdogo huku ukitarajiwa kukamilika mwaka 2024.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi pamoja na kumkabidhi mkandarasi atakayesimamia mradi huo utakaogharimu shilingi Bilioni 7. 11 Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti kutoka REA Nicolaus Moshi amewataka wananchi kutumia fursa ya mradi huo Kuunganishiwa huduma ya umeme.

“Mradi huu ni wa awamu ya Tatu na  kwa hapa Singida na utasambaza umeme katika vijiji miji ,Mradi huu utajengwa katika Kilometa 40.5 Msongo wa kati na mdogo , jumla ya wateja 1802 ambao ni wateja wa awali wataweza kuunganishiwa umeme hivyo wananchi wachangamkie mradi huu ni fursa nzuri na Gharama za mradi huu ni Shilingi Bilioni 7. 11”. alisema Moshi.

Moshi alisema Mradi huo unatajiwa kukamilisha usambazaji wa umeme katika vijiji vilivyopembezoni mwa miji mkoani Singida ndani ya Miezi 18 lakini kwa mujibu wa Mkandarasi wa Mradi huo 'Central electricals international Limited' Kutoka Dar es Salam alisema kuwa atakamilisha kwa muda wa miezi 15.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amesema kuwa vijiji vingi vilivyokuwa pembezoni mwa Miji vilikuwa vinaonekena vimetengwa kutokana na kukosa huduma muhimu za kijamii kama vile umeme maji, afya na elimu.

“Tumepokea mradi wa kusambaza umeme kwa vijiji vilivyopembezoni mwa miji, mradi huu unakwenda kutekelezwa katika vijiji 9 na viyongozji 34 kukamilisha umeme katika maeneo yote yaliyokuwa yanaonekana kuwa yametengwa” Alisema Mhandisi Muragili.

DC Ameongeza kwa Kuwapongeza Wakala wa Nishati Vijijini REA kwa utaratibu mpya  waliyojiwekea wa kuwaweka wazi wananchi miradi inayotekelezwa na kuwataka wananchi kutumia furasa hiyo ili kuepusha gharama kubwa za kuunganishiwa umeme majumbani .

“Niwapongeze sana REA mradi huu tunaunganishiwa kwa Sh. 27000 mradi ukiisha utakabidhiwa Tanesco kama hukuunganishiwa umeme kipindi huki cha mradi sasa utakuja kuunganishiwa kwa Gharama Kubwa uanze kulalamika kwahiyo wakati wao wanaunganisha Nguzo  tuweke nyaya kwenye majumba yetu ili tuinue uchumi, uchumi hauinuliwi kwa kuwasha taa pekee tuchangamkie hii fursa. Tukiwa na umeme ambao hauuziki tunalipa harasa shirika letu”. Aliongeza DC Muragili.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Diwani wa Kisaki Moses Ikaku alisema kuwa ofisi ya mbunge itaendelea kuhakikisha miundombinu inalidwa na kutunzwa ili kuwanufaisha wananchi katika Nyanja za kiuchumi, burudani, elimu , Kilimo na afya lakini itatengeneza ajira kwa vijana wa mkoa wa singida huku Meya Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu alisema kuwa awali wananchi walikuwa wakilalamika umeme kupita maeneo mengine na kusema kuwa mradi huu utachocheza maendeleo kwa wananchi.

 

 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com