Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeitaka Wizara ya Wizara hiyo kufanyia kazi maoni yaliyotolewa na wajumbe wa Kamati hiyo katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu pamoja na migogoro kati ya wananchi na maeneo yaliyohifadhiwa.
Akizungumza
katika kikao cha cha kupokea taarifa ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka (Julai-Desemba,
2022) katika kikao kilichofanyika leo jijini Dodoma ambapo Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Ally Juma Makoa ameipongeza Wizara hiyo kwa kuendelea kutekeleza
majukumu yake yakiwemo yale ya changamoto za wanyamapori.
“Wizara mnafanya kazi nzuri tunaziona,
changamoto zinazoendelea kujitokeza naomba muendelee kuzitatua kwa wakati”, Makoa alisisitiza
Makoa ameitaka
Wizara hiyo kufanyia kazi maoni yaliyotolewa na wajumbe wa Kamati hiyo hususani
katika eneo la kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu
pamoja na migogoro kati ya wananchi na maeneo yaliyohifadhiwa.
“Katika kutatua na kumaliza migogoro
inayotuhusu nashauri tuendelee kutumia busara ili wananchi waweze kuishi kwa
amani na kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi” Amesisitiza Mhe. Makoa.
Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja
ameishukuru Kamati hiyo na kuahidi kufanyia kazi mapendekezo yote
yaliyotolewa ili kuikuza Sekta ya Maliasili na Utalii na hatimaye kuongeza pato
la Taifa.
Miongoni mwa
masuala yaliyojadiliwa ni utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo Mradi wa
Usimamizi wa Maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini (REGROW), Mradi wa
Kukabiliana na Ujangili na Biashara Haramu ya Wanyamapori, Mradi wa Panda Miti
Kibiashara, Mradi wa Kuwezesha Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Nyuki (BEVAC),
Mradi wa Kuongeza Thamani kwa mazao ya Misitu (FORV AC) na ukamilishaji wa
baadhi ya shughuli za Mpango wa Ustawi kwa Maendeleo ya Taifa na Mapambano
Dhidi ya UVIKO-19.
0 comments:
Post a Comment