Na Dotto Mwaibale, Singida.
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima amedhamini na kuzindua
mashindano ya ligi ya mpira wa miguu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) katika Kata ya Minga yajulikanayo
Minga Cup.
Mashindano hayo yaliyozinduliwa jana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Minga
yamelenga kuwaweka pamoja vijana wa kata hiyo sanjari na kuimarisha afya zao
Kwenye uzinduzi huo Mbunge Sima alitoa mpira kwa ajili ya mashindano
hayo ambayo fainali yake inatarajiwa
kuwa Desemba 31, 2022.
Akizungumza na washiriki wa mashindano hayo Sima alisema michezo ni
afya,ajira,upendo,mshikamano na kuwa
inaleta urafiki,umoja,ujamaa,ushirikiano katika masuala mbali mbali.
Aidha Sima aliahidi kuendelea kuwaunga mkono vijana katika jimbo hilo
katika masuala mbalimbali yenye tija ikiwemo michezo.
Katika uzinduzi huo Mbunge Mussa Sima aliongozana na Diwani wa Kata ya Mwankoko, Emmanuel Emadaki.
0 comments:
Post a Comment