MKUU wa wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego,akizungumza wakati akifungua kikao cha nne cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo Novemba 9,2022 Mjini Iringa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ambayeni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa EWURA Mhandisi Modeatus Lumato,akizungumza wakati wa kikao cha Baraza kinachofanyika leo Novemba 9,2022 Mjini Iringa.
KATIBU Tawala Mkoa wa Iringa (kushoto) Mha. Leonard Masanja akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 10 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Iringa, Mhe Halima Dendego, iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ili kuunga mkono utalii wa ndani kupitia tamasha la Utalii Karibu Kusini 2022, linalofanyika mkoani Iringa
MAKAMU Mkuu wa Shule ya Wasichana Iringa( kushoto) Bw. Mikidadi Rashid akipokea mfano wa hundi ya sh. milioni 10 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego(wa pili kulia) iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kusaidia ujenzi wa uzio wa shule hiyo ili kuboresha miundombinu ya kusomea
MKUU wa wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego,(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na vVongozi pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa EWURA mara baada ya kufungua kikao cha nne cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo Novemba 9,2022 Mjini Iringa.
Mkuu wa wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ameielekeza Menejimenti ya EWURA kushugulikia maslahi ya Wafanyakazi kwa wakati ili kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza sehemu za kazi kwa lengo la kuimarisha utendaji na ufanisi wa utendaji.
RC Dendego ameelekeza hayo wakati akifungua kikao cha nne cha baraza la Wafanyakazi wa EWURA , leo 9 Novemba 2022 mjini Iringa.
“Menejimenti ya EWURA kuweni karibu na wafanyakazi wenu, shughulikieni maslahi yao kwa wakati ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima” Alisisitiza RC Dendego.
Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo, amewataka wafanyakazi wa EWURA kuwa na staha wanapodai maslahi yao sanjari na kuwajibika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
RC Dendego pia, alikabidhi hundi yenye thamani ya sh. milioni 10 kwa shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa kusaidia ujenzi wa uzio na shilingi milioni 10 nyingine kuunga mkono juhudi za kuimarisha utalii kwa Nyanda za Juu Kusini katika kushamirisha tamaha la “Utalii Karibu Kusisni 2022”
Akizungumzia msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Modeatus Lumato, alieleza kuwa, EWURA imekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali na kwamba kipindi hiki Mamlaka imetoa kipaumele katika eneo la elimu na utalii.
“Sisi EWURA, tumeona ni vyema tusaidie kuimarisha miundombinu ya elimu pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan katika masuala hayo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa, Mwl Mikodadi Rashid, baada ya kupokea hundi hiyo, aliishukuru EWURA kwa msaada huo na kueleza kuwa utakuwa chachu ya kuboresha mazingira ya kusomea.
Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa Mha.Amani Msuya aliyetoa salamu za TUGHE Taifa kwa niaba ya Katibu Mkuu wake, Henry Mgunda, ameeleza kuwa taasisi zote za umma zinatakiwa kuhakikisha zinakuwa na utaratibu wa kuimarisha maslahi na hali bora za wafanyakazi.
Kwa upande wake Katibu wa TUGHE Tawi la EWURA, Bw. Emmanuel Ndalawa alieleza kuwa, wataendelea kutoa ushirikano kwa menejimenti ya EWURA ili kwa pamoja kuleta tija zaidi katika kuboresha hali bora za wafanyakazi.
Jumla ya wawakilishi wa wafanyakazi 60 wamehudhuria kikao hicho cha nne cha Baraza la Wafanyakazi kitakachofanyika kwa siku mbili mkoani Iringa.
0 comments:
Post a Comment