Rais Dkt Magufuli akizungumza pembeni mwa Rais Yoweli Kaguta Mseven mara baada ya kuwasili mapema mwaka huu. (Maktaba).
Nchi yetu imepata heshima ya kupokea ugeni wa Mhe. Yoweri Kaguta Museven Rais wa Uganda, ambaye anatarajiwa kufika hapa nchini siku ya Alhamisi ya Septemba 5/2019 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia Septemba 5/2019 hadi 07/09/2019.
Mhe. Yoweri Kaguta Mseven atapokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport Terminal I na mwenyeji wake hapa nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli muda wa saa 12.00 jioni.
Mhe. Rais Museveni anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Kongamano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda.
Aidha, Mhe. Rais Museveni anatarajia kuzindua rasmi jengo jipya la Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere lililopo katika Barabara ya Sokoine/Morogoro Dar es Salaam Septemba 6, 2019.
Mgeni wetu anatarajiwa kuondoka hapa nchini tarehe 07/09/2019 na atasindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Tunaomba radhi kwamba njia atakazopitia mgeni wetu zitakuwa zinafungwa kwa muda ili kupitisha misafara ya viongozi wetu wakuu watakaoelekea Uwanja wa Ndege wa Mwl. J. K. Nyerere kumpokea Mgeni wetu hususani barabara ya Nyerere mpaka Mgeni wetu atakapokuwa amewasili na siku ya kuondoka.
Kwa kutambua ugeni huu sisi kama wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania tunamkaribisha mgeni wetu na ajisikie kuwa yuko nyumbani muda wote atakapokuwa hapa jijini.
Wednesday, September 4, 2019
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
-
Ofisi Ya Msajili Wa Jumuiya, Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi imewataka viongozi na wanachama wa vyama, vikundi na taasisi zote zisizo za ki...
-
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Anna Elisha Mngwira akikabidhiwa nyaraka za ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Mkoa mstaafu Mhe Said ...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment