Na Innocent Natai :Arusha
Timu ya mpira wa miguu ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA FOOTBALL CLUB) leo Tarehe 8 Novemba,2022 katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mringa Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha imeendelea kujiada kwa ajili ya kushiriki mashindano ya SHIMMUTA 2022 yatakayofanyika Mkoani Tanga mwanzoni mwa mwezi huu
Akizungumza na WazoHuru Blog, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka Ndg.Remigius Mchunguzi amesema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wachezaji wameonekana kuanza kuzinasa mbinu za Kocha na Kuzifanyia kazi
"Wachezaji wote wameonekana kuwa wenye morali ya kusaka pointi 3 katika kila mchezo unaowajia mbeleni katika michuano hii muhimu, ambazo zitaiweka timu katika mazingira mazuri ya kutwaa Ubingwa" alisema Ndg.Remigius
Aidha ameongeza kuwa Kocha Mkuu amefurahishwa na nidhamu ya hali ya juu kwa wachezaji wake, kwani wachezaji wote wameweza kufanya mazoezi ya leo kwa bidii, na wachezaji wachache ndio wameshindwa kushiriki mazoezi kutokana na majeraha madogo madogo ambayo hayatawaweka nje kwa muda mrefu bali watarejea mazoezini ndani ya siku mbili zijazo
Pia amempongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania Dr Efrem Njau kwa kuakikisha timu inapata mahitaji yote muhimu kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo ya SHIMMUTa yanayotarajia kuanza tarehe 15 Novemba 2022 Jijini Tanga.
0 comments:
Post a Comment