METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, June 28, 2017

WAKAZI WA MTAA WA TAGAMENDA MANISPAA YA IRINGA MIAKA 3 WAKOSA HUDUMA YA MAJI SAFI YA KUNYWA

Wananchi wa mtaa wa Tagamenda katika manispaa ya Iringa wamelalamikia adha ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama ya kunywa kwa kipindi cha miaka 3 huku uongozi wa serikali ya manispaa hiyo ukishindwa kutatua changamoto hiyo jambo linalosababisha wananchi hao kufuata maji katika mto ruaha na kuhatarisha maisha yao.

Wakizungumza na SAYARI YA HABARI iliyofika mtaani hapo na kukutana na baadhi ya wananchi wanaokubwa na adha hiyo ambapo wamelalamikia kutelekezwa na serikali huku wakipigwa porojo ya kutatuliwa kwa kero hiyo walisema wamekuwa wakitafuta maji katika mtoRuaha ambapo maji hayo hutumiwa na wanayama,Kuoga,kufua huku yakitumiwa kwa kunywa binadamu huku vitendo vya kubakwa na kufanyanyiwa kuatili vikitishia maisha yao jambo lililowalazimu wanaume kuanza kuwasindikiza wake zaokutafuta maji.

Sara Edoga ni miongoni mwa Wakazi hao ambao wamekuwa wakipata adha na usumbufu mkubwa kwa kufuata maji na kutumia kutoka mto wa Ruaha alisema amekuwa akibeba maji mgongoni kutokana na umri wake kuwa mkubwa hali inayomfanya ashindwe kujitwisha kichwani na ndipo akapaza sauti.

“hapa tunashida ya maji na Umeme kwa zaidi ya miaka 3 tunatumia maji ya mto Ruaha tunatia huruma tumetelekezwa kama kisiwa kwa umri wangu nalazimika kubeba mgongoni maji wakati yamepita hapo chini shule ya Sekondari Tagamenda tuoneeni huruma mbona tupo manispaa”alisema mama huyo kwa huruma

Naye Willium Fungo ni mzee wa mtaa huo kwa uchungu alisema kumekuwa na kauli za baadhi ya viongozi wanaosema eneo la Mtaa wa Tagamenda ni eneo la milimani hivyo hawawezi kupatiwa huduma ya maji jambo linalowafanya wajiulize maswali iweje kauli hizo ikiwa kodi za majengo zinatozwa?akaongeza kusema kasi ya ukuji wa mtaa huo ni kubwa wapo karibu na kituo cha Shirika la Umeme TANESCO lakini hawana pia umeme jambo linalowakatisha Tamaa kushiriki katika shughuli za maendeleo.

“hatuna maji,hatuna Umeme zote ni shida zetu zinatukabili,sasa kuna utaalamu fulani um ekuja wa kusema tuweke maji chooni hivi utaweka maji wakati hayapo na msishangae kuja hapa mnakuta watoto wachafu yote hii ni kwa sababu ya kukosa maji tunateseka sana heri tukose chakula lakini tupate maji safi ya kunywa”alisema mzee huyo

Kwa upande wao baadhi ya Madiwani Dora Nziku vitimaalum ,Bashir Mtove na Mahadhi Hepautwa walizuru katika mtaa huo ili kujionea adha wanayoipata wananchi hao wamesema richa ya mateso na shida wanazozipata za kukosa maji lakini wao kwa umoja wao wamewahakikishia kushughulikia kero hiyo ili kuwaokoa wanawake na vitendo viovu.

“nikweli sisi ni madiwani kutoka kata tofauti tofauti mara baada ya Kusikia kilio cha wananchi hawa ambao ni walipakodi katika Manispaa yetu Tumeamua kufika ili tujionee wenyewe na tuchukue hatua ya kuwasaidia tumeo hali hii siyo nzuri hata kidogo wapo kama kisiwani tuwaahidi wananchi hawa kuwa kero hii sasa imefika mwisho” walisema

Hatimaye Mbunge wa Vitimaalumu mkoani Iringa Rita Kabati akajitokeza na kuzungumzia changamoto hiyo huku akishangazwa na kauli za baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakidai kuwa katika manispaa ya Iringa hakuna Tatizo la ukosefu wa huduma ya maji na kuwaahidi kuitatua kero hiyo katika kipindi cha muda mfupi ujao.

“nimekuja huku kwa masikitiko makubwa kwani ninaposikia kero ya maji naumia ninapomuwazia mwanamke mwenzangu anayepata adha na kodi analipa na anakabiliwa na vitendo vya ubakaji kwa kufuata maji umbali mrefu imeniuma sana kwanini tunawadanganya wananchi waendelee kupata shida hizi mimi kama kiongozi naanza leo kufuatilia kero hii hapa mnahaki ya kupata maji kama wanavyopata watu wengine mnayo haki ya kupata umeme tena kwakuwa upo karibu hapa.”alisema Kabati

Mtaa wa Tagamenda una zaidi ya kaya 30 na upo umbali wa kilomita 2 kutoka kilipo kituo cha mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Iruwasa na mita 800 kilipo chanzo cha umeme wa TANESCO cha Tagamenda lakini mtaa huu hauna maji wa Umeme hali inayowapa shida wananchi na kuwa hatarini kuugua maradhi kutokana na kutumia maji yasiyo salama.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com