Serikali kupitia Wizara Ya Viwanda Na Biashara imeanzisha tuzo za ubora kitaifa ikiwa ni mpango wa kuboresha bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini ili kuhakikisha mifumo,bidhaa na huduma zinakidhi ubora kitaifa ,kikanda na kimataifa.
Kaimu Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Uwekezaji Viwanda Na Biashara Aristides Mbwasi amesema hayo jijini Dodoma wakati akizindua tuzo za tatu za ubora kitaifa kwa taasisi na watu binafsi wanaofanya vizuri kwenye masuala ya ubora kwa mwaka 2022/2023
Amesema mashindano ya Tuzo hizo ni pamoja na Tuzo kwa kampuni bora , tuzo kwa bidhaa bora , tuzo kwa huduma bora , tuzo kwa muuzaji bora wa bidhaa nje ya nchi na mtu mmoja aliyefanya vizuri kwenye masusla ya ubora .
Pia amesema mashindano hayo wadau watapata fursa ya kufahamika zaidi kwenye jamii na kushiriki kwenye mashindano ya tuzo za ubora kwa jumuia ya Afrika Mashariki , mashundano ya tuzo za ubora kwa nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika na kufahamika kupata masoko zaidi.
"Serikali kupitia wizara ya uwekezaji ,viwanda na Biashara iliona umuhimu wa kuanzisha tuzo hizi na kutoa jukumu la kuziratibu kwa shirika la viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na sekta binafsi nchini (TPSF) Taasisi ya viwango Zanzibar , shirikisho la wenye viwanda nchini ,"
" Pia tumeshirikiana na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini (SIDO) ,chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania , Chemba ya Biashara , viwanda na Kilimo Tanzania na mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania "amesema Mbwasi.
Hata hivyo amewataka watanzania kuwa mabalozi wa Kuhamasisha wazalishaji wa Bidhaa na watoa huduma kushiriki mashindano ya Tuzo za ubora za mwaka 2022/2023.
Nae Mkurugenzi mkuu wa shirika la Viwango Tanzania Daktari Athuman Ngenya akizungumzia maandalizi yalivyo mpaka alisema kuwa yanaendelea vizuri kwa kutumia warsha mbalimbali na vyombo vya habari ,mitandao ya kijamii ambapo yatasaidia kuwapata washindi.
"Katika maandalizi haya tumewapa kipaumbele akina mama wajasiliamali kuwahamasisha ili waweze kushiriki kwani ni wengi ambao wamejikita kwenye ujasiliamali." Alisema Ngenya.
Kwa upande wake Hafsa Ali Slim Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwango ambapo akimuwakilisha Mkurugenzi ZBS
alisema kuwa wanatarajia kutoa uelewa kwa wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa upande wa Zanzibar ili waweze kushiriki kwa wingi zaidi.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment