METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, August 12, 2022

MATUKIO KATIKA PICHA CHONGOLO ZIARANI MKINGA TANGA

  

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Chuo Cha Veta Mkinga kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Veta Tanga Ndugu Gideon Ole Laiombe (kulia), kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkinga Ndugu Ismail Kasomo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Hassan Surumbu mara baada ya kuwasili wilayani hapo akitokea wilaya ya Pangani, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Ndugu Ghalibu Ringo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Mwenyekiti wa shina namba 3 tawi la Mapambano Ndugu Mnyatani Msema (kulia) mara baada ya kutembelea na kuzungumza na wakazi wa shina hilo lililopo Kijiji cha Magani wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakazi wa shina namba 3 tawi la Mapambano Kijiji cha Magani wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com