WANANCHI wa Wilaya ya Momba mkoa wa Songwe wamefarijika baada ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa daraja la muda katika mto Nkana uliopo Kata ya Chilulumo.
Hatua
hiyo imechukuliwa baada ya daraja la awali kuvunjika na kusababisha mawasiliano
ya Kata za Chilulumo,Nkulwe,Kamsamba,Mkomba Ivuna na makao makuu ya Wilaya ya
Momba kukatika.
Akitoa
taarifa kwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TARURA, wakati wa ziara yao mkoani Songwe,
Meneja wa TARURA Mkoa wa Songwe Mhandisi Killian Haule alisema kuwa TARURA kwa
kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Songwe,Jeshii la wananchi wa Tanzania
(JWTZ), wamejipanga kurejesha mawasiliano ndani ya muda mfupi kwa kujenga
daraja la chuma (TRUSS Bridge) ili wananchi wapate huduma ya Usafiri na
Usafirishaji.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA Mhandisi Florian Kabaka amesema kuwa
daraja hilo ni muhimu sana kwa uchumi wa wananchi na amewataka wananchi
kulitunza pindi litakapo kamilika.
Mkurugenzi
wa barabara kutoka TARURA Mhandisi Venant Komba ameeleza kuwa licha ya ujenzi
wa daraja la muda, TARURA inafanya maandalizi ya ujenzi wa Daraja la kudumu
katika mto Nkana.
"Maandalizi ya ujenzi wa daraja
la kudumu hapa mto Nkana yanaendelea maana eneo hili ni muhimu sana kwa
wananchii ili kuwawezesha kusafirisha mazao hasa zao la mpunga,”
alisema mhandisi Komba.
Kwa
upande wake Mhe. Sabasi Semfukwe, diwani wa kata ya Chitete alisema kuwa
walikuwa wanapata changamoto kubwa sana kutokana daraja kuvunjia, kwa
kuzingatia kuwa njia hiyo ni ya kimkakati kwa ukuaji wa uchumi wa maeneo yao.
“Tumefarijika sana sababu kujengwa kwa daraja hili kwetu ni
kufungua ukuaji wa kiuchumi kwa kusafisha mazao yetu. Mawasiliano sasa
yatakuwepo na itaongeza tija kwa wananchi katika maswala ya uzalishaji,”
alisema Mhe. Semfukw.
Naye Rehema Kipubile mkazi wa Kanyala alisema kuwa
anaishukuru Serikali kwa kuwaletea daraja hilo kwani wamepata tabu sana baada ya mawasiliano
kukatika kuzifikia huduma muhimu za kijamii.
“Sisi wakinamama hasa tukiwa
wajawazito tumepata tabu sana kuvuka hapa kwenda hospitali, tunashukuru sana
kwa daraja hili jipya linalojengwa tutapata nafuu,
“ alisema Rehema
Bodi
ya Ushauri ya TARURA imekamilisha ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi
katika Mikoa ya Iringa,Mbeya na Songwe ambapo imeridhishwa na kasi ya
utekelezaji wa miradi na kuleta matokeo chanya ndani ya kipindi cha miaka
mitano tangu kuanzishwa kwa wakala
0 comments:
Post a Comment