Na Okuly Julius-Dodoma
Bodi ya usajili wa ubunifu majengo na wakadiriaji majenzi (AQRB) imesema kuwa watatumia vyema Maonesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) 2022 kukutana na wanafunzi wa vyuo, sekondari,shule za msingi na wadau wengine mbalimbali ili kuhamasisha umuhimu wa kusoma masomo ya sayansi.
Lengo la kuwahamasisha umuhimu wa kusoma masomo ya sayansi ni kuendana na soko la ajira hasa kwa upande wa ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi kwa sababu ni moja ya kazi inayohitaji ubunifu mkubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Banda la Bodi hiyo katika maonesho hayo yanayoendelea katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma AFISA UHUSIANO wa Bodi ya Usajili wa ubunifu majengo na wakadiriaji majenzi ATUGONZA SAMWEL amesema kuwa wanafaidi sana kushiriki katika maonesho haya kwa sababu wanapata fursa ya kukutana na wadau pamoja na kuwapa ushauri kuhusu masuala ya ubunifu na ukadiriaji majenzi.
''Bodi inafanya kazi kubwa sana na baadhi ya kazi ambazo bodi inazifanya ni kusajili kazi za ujenzi wa majengo,kutembelea na kukagua sehemu inapofanyika shughuli za majenzi na kuhakikisha kwamba shughuli zote zinazobuniwa zinasimamiwa na makapuni ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi waliosajiliwa na boda na kuhakikisha kazi hiyo zinakidhi na zinafuata sheria za nchi,kutoa ushauri kwa jamii na kuandaa mashindano ya ubunifu wa majengo'' Amesema Atugonza
Pia amesema kuwa lengo la Bodi kwa mwaka huu ni kuongeza idadi kubwa ya wasichana ili kuweka mlinganyo mzuri kwani mpaka sasa fani hii ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi inadadi ya wanaume ni kubwa sana ila kwa sasa kupitia maonesho mbalimbali matokeo yanaonekana kwani wasichana wameanza kujitokeza.
Kwa upande wake Mbunifu Mjengo Mwandamizi wa Bodi hiyo PANTALEO MWAMBA amesema kuwa bodi hiyo ni chomba cha serikali ambayo imepewa majukumu ya kuratibu utendaji wa wabunifu wa majengo na wakadiriaji majenzi pamoja na taaluma ambayo inashabihiana nao.
Pia bodi hiyo ina kazi kubwa ya kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kutumia wataalamu katika ubunifu wa majengo na ukadiriaji wa majenzi ili kuendelea kuweka ufanisi katika sekta ya ujenzi.
''Tunatoa ushauri tumieni wataalamu katika ujenzi kwani ni muhimu kwa maslahi ya nchi pamoja na kazi mnazofanya na muhakikishe makapuni mnayotumia yawe yamesajiliwa na bodi'' Amesema Pantaleo
Ametoa wito kwa wananchi kutembelea Banda lao ili kupata elimu , kuna faida kubwa sana ya kwa sababu ujenzi unahitaji ubunifu na wabunifu wa majengo wanapatikana (AQRB)
0 comments:
Post a Comment