![]() |
Timu ya SMAUJATA ikiongozwa na Mwenyekiti Bwana Vicent Mafuru wakizungmza na walimu wa shule ya viziwi Tumaini Iliyopo Manispaa ya Singida ili kuanza kutoa elimu ya kukabiliana na ukatili |
![]() |
Wanafunzi wa shule ya viziwi Tumaini wakishangalia kwa furaha wakati wakipata mafunzo walipotembelewa na SMAUJATA mkoa wa Singida. |
![]() |
Walimu wakifuatilia kikao cha Smaujata Ofisini Kwao mapema hii leo. |
![]() |
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida Akimvalisha Badge ya kampeni hiyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Tumaini ya watoto wasio sikia |
![]() |
Walimu na Timu ya SMAUJATA wakiwa katika Picha ya Pamoja baada ya Mazungumzo hii leo |
![]() |
Katibu wa kamati ya Ufuatiliaji ya SMAUJATA Mkoani Singida Bi. Elizabeth Samike akimvisha Beji ya Kampeni hiyo Mkuu wa shule Msaidizi wa Tumaini Rosemary Justine Kiwale. |
![]() |
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida akimpa mkono Mwalimu Mkuu wa Shule ya Tumaini ya watoto wasio sikia baada ya kumvalisha Beji ya kampeni hiyo shuleni hapo. |
Na
Hamis Hussein – Singida
Kampeni ya Shujaa wa maendeleo na Ustawi wa jamii
Tanzania SMAUJATA imepanga kuyafikia makundi maalum ya watoto wasio sikia na
kuona walioko mashuleni Mkoani Singida kuwapa elimu ya jinsi ya kuripoti na
kukabiliana na vitendo vya ukatili katika jamii yao ikiwa ni lengo la
kuutokomeza ukatili ili kuwa na jamii endelevu .
Smaujata mkoani hapa imefika katika shule ya watoto wasio sikia yaani viziwi
iliyopo Manispaa ya Singida na kuueleza
uongozi wa shule hiyo juu ya kampeni hiyo ambayo imeanza kuifikia jamii na
kuielemisha juu ya ukatili na masuala mbalimbali ya maendeleo baada wiki
iliyopita kuzinduliwa rasmi kitaifa.
Akizungumza na viongozi wa shule hiyo ya Viziwi
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida Vincent Mafuru alieleza shabaha ya wao
kutaka kutoa elimu kwa makundi maalum ya watoto wakiwemo wenye ulemavu wa
masikio na macho ambapo alisisitiza kuwa kundi hilo linawezakuwa
linakumbana na ukatili lakini likashindwa kutoa taarifa ili kupata msaada.
"Tunahitaji
kuyafikia makundi tofauti tofauti,tumeshaanza mashuleni tumeunda Vilabu
vya watoto, tumejaribu kuwaelimisha
namna wanavyoweza kujimudu katika mazingira ambayo ukatili unatokea pia
tumelifikia kundi la bodaboda tunawaambia ukatili Sasa ufikie kikomo"
alisema Mafuru akiongea na Walimu na wanafunzi wa Shule ya Viziwi Tumaini
mkoani Singida.
Kuhusu kuyafikia makundi maalumu ya watoto Mwenyekiti
huyo wa Smaujata mkoani Singida Mafuru alisema kuwa kundi lingine la muhimu
kulipatia elimu ya kuripoti na kukabiliana na ukatili ni Kundi la watoto wasio
sikia na wale wasioona.
"Tumeona
tufike hapa (Tumaini) tuongee na ninyi ili tuone namna ya kuwaelimisha watoto
wetu juu ya ukatili unaotendeka kwenye jamii zetu ili waone kuwa mazingira hayo
ya ukatili hayana nafasi tena" aliongeza Mafuru.
Mkuu wa shule hiyo ya Tumaini Mwalimu Francis Damian
aliishukuru kampeni hiyo kubisha hodi katika familia hiyo na kusema kuwa elimu
watakayoipata watoto itakurahisi hata walimu ambayo ni walezi wa watoto
kuweza kuwasiadia pindi wanapofanyiwa ukatili.
"Tunashukuru
mmeona na sisi tuko katika jamii, Hawa watoto wanaweza kuwa wanakumbana na
ukatili lakini wanakosa mahali pa kuelezea, hivyo elimu hiyo itarahisisha
wao kujilinda na hata kama bahati mbaya wamekumbana na ukatili nitakuwa rahisi
kwa sisi walezi wao kujua" alisema Mwl.Francis
Mwalimu Francis ametoa siku ya ijumaa ya kila mwezi
Smaujata kwenda kutoa elimu ya kukabiliana na ukatili ambapo itakuwa kuanzia
saa 10:20 asubuhi hadi saa 12:20 mchana
Kuhusu malezi ya watoto alisema watoto kulala na ndugu
wanaowatembelea wazazi ni miongoni mwa sababu inachangia ukatili dhidi ya
watoto na kuonyesha kero kwa walezi wenzake wanaofanya ukatili kwa watoto akitolea
mfano baadhi ya walimu .
"Watoto
kulala na ndugu ambaye amekutembelea nyumbani unakuwa na hofu kwa sababu
yanaweza kutokea Yale tunayoyasikia lakini yule Mwalimu aliyewafanyia ukatili
wanafunzi ametudhalilisha sana anafundisha huku akiwaharibu, watoto kumbe hata
sisi walimu tuna matatizo ,hivyo hakuna mtu wa kumuamini moja kwa moja kwamba anaweza kumlinda mtoto hiyo elimu
hiii iwe na utashi kwa mapana yake"
aliongeza mwalimu Francis.
0 comments:
Post a Comment