METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 3, 2022

RC MAKALLA ATOA SIKU 14 KWA WAVAMIZI WA ARDHI MBONDOLE KUONDOKA

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa muda wa siku 14 kwa Wananchi zaidi ya 700 wa Mtaa wa Mbondole Wilaya ya Ilala waliovamia na kujenga kwenye eneo la Mzee Martin Nasson kuondoka na kutoa wito kwa Wananchi kuacha tabia ya kuvamia maeneo.

RC Makalla ametangaza maamuzi hayo Baada ya Kukosekana kwa muafaka baina ya Mmiliki aliepewa haki na Mahakama kushindwa kukubali ombi la Wavamizi waliotaka kumlipa fidia ili waachwe kwenye eneo Hilo.

Kutona na Hilo RC Makalla amesema ifikapo Tarehe 18 mwezi huu asionekane mtu kwenye eneo Hilo na kusisitiza kuwa siku 14 zilizotolewa ni Huruma ya Serikali kwakuwa tayari walishaamuriwa na Mahakama kuondoka tokea muda mrefu.

Hata hivyo RC Makalla Serikali itaendelea kuheshimu Maamuzi yanayotolewa Muhimili wa Mahakama katika kusimamia Sheria.

Pamoja na hayo RC Makalla amewatahadharisha Wananchi kuacha tabia ya kuvamia au kununua maeneo pasipo kujiridhisha na Nyaraka za umiliki.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com