Na Fredy Mgunda, Iringa.
Wananchi wa Kijiji cha Luganga tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa wamemkataa diwani wa kata ya Ilolo mpya Fundi Mihayo kuwa sio kiongozi wao tena kutokana na kuhujumu maendeleo ya wananchi hao.
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara mbele ya mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo walisema kuwa amekuwa anaongoza kwa kutumia mabavu na kupora miradi ya jumuiya.
Anjelista Pinda ni mwenyekiti wa skimu ya UKULUPA alisema kuwa umojaa kilimo cha Umwagiliji ya Luganga Pawaga UKULUPA Umedai kupata hasara kiasi milioni kumi kwa mwaka 2020/21 kutokana na migogoro ya mara kwa mara baina ya uongozi wa skimu na diwani wa kata ya Ilolo mpya
Pinda alisema kuwa Mapato ya skimu yamekua yakisuasua tangu migogoro wanayodai kuwa imesababishwa na Diwani huyo ikiwemo kupora jukumu la ukusaji wapato na kulikabidhi jukumu hilo kwa serikali.
Alisema kuwa diwani huyo amekuwa akitumia madaraka yake vibaya kwa kuwalazimisha wajumbe wa skimu hiyo kumpa fedha kinyume cha sheria za skimu na ndio chanzo cha mgogoro baina ya wananchi wa Kijiji cha Luganga na diwani Fundi Mihayo.
Pinda alisema kuwa baada kuona wajumbe wa skimu hiyo wameanza kukataa maagizo yake ndio alipoamua kuunda timu mpya ya kusimamia skimu hiyo kinyume na sheria za tume ya umwagiliaji.
Alisema kuwa uongozi wa skimu hiyo ulipoisha muda wake ilitakiwa kufanyike uchaguzi kwa mujibu wa katiba waliyonayo iliyopitishwa na time ya umwagiliaji taifa lakini kwa kutumia mabavu alikataza hakuna kufanyika kwa uchaguzi wowote jambo ambalo ni kinyume na katiba ya skimu hiyo.
Katika
mkutano huo wa hadhara wananchi waliibuka na kudai kuwa diwani huyo
hawafai kwa kuwa amekuwa anatumia madaraka yake vibaya kwa kuaatisha
wananchi,kutowasikiliza,
Walisema kuwa uongozi wa polisi kata watendaji wote wa kata na vijiji hawafanyika kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi bali wanafuata maelezo Kutoka kwa diwani jambo ambalo linapelekea wananchi wengi kunyanyaswa na kunyimwa haki zao za msingi kijijini hapo.
Kwa kauli moja wananchi hao walimuleza mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo kuwa hawataki tena kuongozwa na diwani huyo ambaye amekuwa anatumia mabavu,unyonyaji na kuwanyima haki wananchi wakati akiwaongoza.
Walimalizia kwa kumuomba mkuu wa wilaya ya Iringa awalinde maana akiondoka tu watakamatwa na kuwekwa ndani na diwani kupitia mtendaji na jeshi la polisi la kata na tarafa hiyo.
Kwa upande wake Katibu wa umoja wa skimu hiyo Boss Mongo anasema Diwani amekuwa akiwatishia pindi wanapohitaji kufanya uchaguzi akidai kuwa lengo lake ni kupandikiza watu anaowataka kinyume na muongozo wa katiba
Mongo alisema kuwa baada ya kuona diwani huyo anatumia vibaya madaraka yake waliamua kukata mlija wa kumpa fedha ndio alipoamua kuanzisha mgogoro ambao hauna msingi wowote ule kwa afya ya wananchi wa Luganga.
Alisema Endapo Serikali ngazi ya wilaya na mkoa kwa ujumla haitoingilia kati Umoja huo hautoweza kuendelea
Akijibia
malalamiko hayo ikiwemo vitisho dhidi ya viongozi wa Skimu, Diwani wa
kata ya Ilolo Mpya Fundi Mihayo licha ya kukanusha amesema Serikali
ilisitisha baadhi shughuli za Skimu hiyo baada ya kubaini ubadhirifu
katika utendaji wake
Mihayo alisema kuwa viongozi wa skimu hiyo na baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho wamekuwa wanatumika kisiasa kumchafua kwa ajili ya chaguzi zijazo kwa kuwa miongoni mwao amekuwa anawashinda mara kwa mara.
Lakini diwani huyo alishindwa kudhibitisha ubadhirifu wa viongozi waskimu hiyo kwa kuwa hakuwa na na vielelezo vya madai ya ubadhirifu aliowatuhumu viongozi wa skimu hiyo.
Diwani Fundi Mihayo alisema kuwa wananchi wa Kijiji cha Luganga sio wapiga kura wake hivyo kuona wanatoa tuhuma hizo ameshawazoea ndio maana amekuwa hapati kura kipindi cha uchaguzi Kutoka kwa wananchi wa Kijiji hicho
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo alisema kuwa Serikali imesikia kilio na kuwaomba wananchi wawe na utulivu anaunda tume maalumu kushughulikia kero za wananchi pamoja na skimu hiyo ili wananchi waweze kufanya shughuli za kimaendeleo kama walivyokuwa wanafanya awali.
Moyo alimuagiza mtendaji wa kata kutoa maelezo kwanini uchaguzi haufanyiki katika skimu hiyo na nani alitoa idhini ya kusimamisha uchaguzi wa skimu hiyo ili ajue aanzie wapi kutatua changamoto hiyo.
Alisema kuwa viongozi wa kata ya Ilolo mpya wanatakiwa kutumia busara kwenye maamuzi mbalimbali ambayo wanakuwa wanayachukua kwa wananchi waliowachagua na wanaowaongoza ili wote wawe wamoja kuwa wanajenga nyumba moja.
Moyo alimuagiza mtendaji wa kata,mkuu wa kituo cha polisi na afisa tarafa wa pawaga kuwa wakimuweka ndani mwananchi ni lazima wakamfungulie mashtaka mahakamani mwananchi huyo na sio kuwaonea wananchi kwa kuwa wao wamepewa madaraka hayo.
Alimazia kwa kuwaomba wananchi wasiwe na hasira na viongozi hao kwa kuwa ameyasikia yote anayatufutia ufimbuzi na hakuna mwananchi ambaye atanyanyaswa tena na ikitokea kiongozi anamnyanyasa mwananchi wampigie simu kwa kuwa alishawapa namba yake ya simu kumaliza mgogoro mbalimbali ya wananchi hao.
0 comments:
Post a Comment