METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, April 15, 2022

ARUSHA KUPOKEA NAKALA 113,308 ZA VITABU VYA KIADA KWA SHULE ZA SEKONDARI VINAVYOTOLEWA NA TAASISI YA ELIMU TANZANIA

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania inaendelea na zoezi la usambazaji wa vitabu vya Kiada kwa shule za Sekondari. 

Leo tarehe 15/04/2022 jumla ya nakala 113,308 za vitabu vya Kiada mwa shule za Sekondari zinasafirishwa kuelekea Mkoani Arusha.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Aneth Komba huku akisisitiza kuwa serikali inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan imekusudia kuimarisha sekta ya elimu.

Vitabu hivyo vitasambazwa kwenye Halmashauri 7 za Mkoa huo ( Arusha DC, Arusha CC, Karatu, Longido, Meru, Monduli na Ngorongoro)

Zoezi la usambazaji linafanywa kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)

Zoezi la ugawaji wa vifaa na vitabu vya Kidato cha 1-6 vya Braille na Maandishi yaliyokuzwa kwa ajili ya mwanafunzi wenye mahitaji maalumu ya kutokuona na uoni hafifu nchini vilivyoandaliwa kupitia mradi wa mpango na matumizi ya fedha za maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO-19 lilizinduliwa Jijini Dar es salaam tarehe 5 Aprili 2022 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda.

Waziri Mkenda alisema kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilipokea kiasi cha bilioni 64 kwa ajili ya mradi wa maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO 19. Kupitia mradi wa mpango huo, Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 707,000,000/- kwa ajili ya kuchapa vitabu vya kiada kwa matumizi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Kadhalika alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kujali na kuthamini elimu ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Kwa kutumia fedha hizo kwa mara ya kwanza katika historia Wizara imeweza kuandaa vitabu vya sekondari vya maandishi ya Braille li na yaliyokuzwa kwa matumizi ya wanafunzi ngazi ya elimu ya sekondari Kidato cha 1-6.

Fedha hiyo imeweza kuchapa jumla ya nakala 9,100 ya vitabu vya Braille vyenye jumla ya juzuu 32,140 pamoja na vitabu vya michoro mguso vyenye jumla ya juzuu 20,400. Vitabu hivyo ni maalumu kwa ajili ya wanafunzi wasioona. Taasisi ya Elimu Tanzania imeweza kuchapa vitabu vya kiada vya Maandishi yalikuzwa nakala 60,283 kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu. 

MWISHO
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com